SOMO: NGUVU (MCH. CONSOLATA KITUNDU – WA HUDUMA YA EFATHA MKOA WA TANGA)

Mch. Consolatha Kitundu

Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,”
-Katika kutimiza malengo yako, zipo changamoto na maumivu ambayo utakutana, yatupasa kuvumilia na kuyastahimili maumivu utakayokutana nayo.
-Ili kutimiza malengo hayo ni lazima uwe na Nguvu ya Mungu itakayo kusababisha wewe kushinda katika kila changamoto utakazokutana nazo, maana shetani yupo ili kuzuia malengo yako yasitimie.
-Tambua kwamba unapopanga kuazimisha jambo lako, mfano biashara au kilimo, juwa wazi kuwa shetani nae anapanga kuharibu mipango yako ili usifanikiwe.
-Yatupasa kuwa na Nguvu ya Mungu kutimiza kila mpango katika maisha yetu.
-Yapo mambo ambayo shetani anaweza kuyatumia ili kuharibu mipango yako.
Roho ya kukata tamaa.
Waebrania 12:3 “Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.”
-Wakati upo katika kukamilisha malengo na mipango yako, shetani atakushambulia katika kila cheo la mipango yako ili akutakatishe tamaa.
-Ukikata tamaa huwezi kufanya jambo lolote.

Mithali 24:10 “Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.”
-Bila Nguvu ya Mungu ni lazima utazimia moyo,
Ili kukaa na Nguvu ya Mungu ni lazima ujue.
I. Baini umeitiwa nini.
II. Unafanya ulichoitiwa kwa usahihi.
III.Unafanya ulichoitiwa na Mungu kwa moyo WA kupenda.
IV. Unalijua Neno la Mungu.

UJUMBE: NEEMA – MCH. MICHAEL G. KUSWA (EFATHA MINISTRY MBEYA)

Warumi 8:14 “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. “

Kurithi kunakupa utoshelevu.palipo na Neema panakupa urithi na urithi unakupa kua mtoshelevu.

Palipo na Neema pana ufadhili, Ukiwa na Neema Mungu yupo ili kukufadhili.

2 Nyakati 17:3-5 “Naye Bwana alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye, asiyatafute mabaali;
4lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli. Kwa hiyo Bwana akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na Yuda wote; basi akawa na mali na heshima tele. ”

Neema inakupa kutenda ya Mungu .Neema itakupa kutenda yale ya Mungu. Palipo na Neema pana utoshelevu na utele.

2 Nyakati 1:7-10 “Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee Bwana Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye “

Roho wa kumcha Bwana atakusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.

2 Nyakati 9:22 “Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima. “

Palipo na Neema ya Mungu pana utukufu mwingi.Na mtu yoyote aliye na Neema amezungukwa na utukufu, Neema ikiwepo na Utukufu unakuwepo. Kama mtu ana Neema na utukufu umemzunguka..mtu huyu haishi kwa Imani bali anaishi kwa kuelewa. Neema inakutoa kunako Imani na unaanza kuishi kwa ufahamu na sio tena kwa imani maana utukufu wa Bwana umekuzunguka.

Kwenye Neema kuna kujibiwa maombi yako. Na kama eneo lina neeema basi maombi ya watu yatajibiwa.
Palipo na Neema maombi yanajibiwa kama Efatha tulivyo tuna Neema ndio maana maombi yetu yanajibiwa. Neema ipo ili kuimarisha na kuthibitisha maombi yako. Kwa hivyo unahitaji kuwa katika hali ya Neema ili maombi yetu yapate uthibitisho kwa Bwana.

Palipo na Neema pana ulinzi, ukiwa na Neema unalindwa. Neema ipo ili kukufanya wewe mtu wa Ibada na kukufanya wewe mtu wa ibada. Neeema inakupa kufanya ibada ya kumfurahisha Mungu, mpe Bwana Ibada iliyo kamili ili Bwana apate Kufurahishwa na Ibada ya moyo wako. Ukimfurahisha Mungu naye atakufurahisha.yoyote mwenye Neema anaaminiwa na Mungu; Mungu anakua na uamini wa kumpa mtu huyo mali.

Mtu mwenye Neema anakua kila iitwapo leo sio kiroho bali ni kimaendeleo, ukijichunguza na ukijua kua hakuna kitu kilichoongezeka hapo ujue kua Neema imepunguka kwako, Kile kitu kinachoweza kukusaidia icho kitakupa ongezeko. Neema inakupa kuongezeka, Mungu hamwamini kila mtu bali anamwamini mtu yule mwenye Neema tu.

Neema inamfanya Mungu akuamini na kukukabidhi mali zake ili uwe kituo cha ugawaji.

MWENE NEENA SIYO MCHOYO..

Mwenye Neema anahuruma ya Mungu na mtu huyu anahitaji sana roho ya shauri ili apate ushauri juu ya watu wa kuwahurumia.

Ukiwa na Neema Mungu anakufanya kua kituo cha ugawaji kwa wale ambao anakuelekeza au anakuambia juu ya habari ya ugawaji.

Neema inakupa kumcha Bwana ,utukufu wake unakuzunguka na ule ukuu wake unakua ulinzi kwako na familia yako.

PALIPO NA NEEMA PANA UVUMILIVU AU HESHIMA

MTU MWENYE NEEMA ANAHESHIMIKA.

MFANO : MSIBA WA MASIKINI WATU WANAO HUDHURIA NI WACHACHE SANA KULIKO WALE WANAOKUFA MATAJIRI …WANAOKUFA MATAJIRI MISIBA YAO INAFURIKA WATU KWASABABU TAJIRI HUYO AMESAIDIA WENGI.NA MSIBA WA TAJIRI HUYU KUNAKUA NA HESHIMA NA UNAONGELEWA VIZURI KWASABABU YA HELA ZA YULE TAJIRI .

UKIFA MASIKINI AU OMBA OMBA MSIBA WAKO UNAWEZA UHUDHURIWE NA WATU KUMI MAANA UNAKUFA NA HAUJAMSAIDIA MTU..PIA MSIBA HUU UTASEMWA KWA MENGI KWASABABU MTU HUYU AMEKUFA BILA HELA NA PIA HAKUNA ALYESAIDIWA NA MAREHEMU .

* UMASKINI NI MBAYA.

* UKIRI.BWANA YESU NAHITAJI HELA ILI NEEMA YAKO IKAE NAMIMI.

* UNAHITAJI NEEMA SANA .

MUNGU AKIKUPA NEEMA…NEEMA HIYO INAKUNEEMESWHA.

TUJIFUNZE KWA TAI NA TABIA ZAKE – (EFATHA MINISTRY USA RIVER)

Mchungaji: Baraka Lymo

Nguvu ya Mungu ipo kwaajili ya kufanya mambo makubwa. Kama unataka kufanya mambo makubwa basi leo mkono wa Bwana upo pamoja na wewe, Mkono wa Mungu uko na wewe saa hii

Waliokukataa mwaka huu lazima wakukubali, Kama ulifukiwa shimoni lazima ufukuliwe kutoka kwenye hilo shimo saa hii, Nipo mahali hapa kwenye madhabahu hii kukwambia kile Mungu anaenda kufanya kwako.

Mtu yeyete mwenye Nguvu za Mungu anafananishwa na Tai, mtu mwenye mawazo ya juu anafananishwa na tai. Tai Ni Ndege anaye ruka juu sana, Tai ana Kg 4 lakini anaweza akabeba mzigo wa kg 20 na akautoa mahali na kupeleka mbali, hivyo husijidharau kwa kuangalia mazingira yako.

Tai ana uwezo mkubwa wa kuona, anaweza akaona fursa ambazo wengine hawawezi kuona. Nguvu ya Mungu inakuja tu kwa wale walio na macho kama ya tai.

Tai anatabia ya kufundisha watoto wake na Tai mkubwa wa Efatha ni Josephat E. Mwingira, anatufundisha kila iitwapo leo

Je wewe ni tai? Mambie Mungu saa hii NAITAKA NGUVU YAKO siku ya leo.

KARIBU KANISANI EFATHA MINISTRY USA RIVER, KANISA LIPO LEGANGA USA RIVER ARUSHA WILAYA YA MERU, SHUKIA STAND YA POSTA, HALAFU FUATA NJIA HADI SHELI ILIYOKARIBU NA POSTA, KISHA KUNA NJIA NG’AMBO YA SHELI (YAANI UKIVUKA BARABARA), FUATA HIYO NJIA HADI MWISHO UTAKUTANA NA JENGO LETU MAHALI LILIPO…AU UKISHUKA LEGANGA, ULIZIA KANISA LA EFATHA MINISTRY LILILO JUU YA NDESAMBURO LODGE, UTAFIKISHWA…WOTE MNAKARIBISHWA…

Kwa Msaada zaidi wasiliana na Mchungaji kwa simu: 0763 480 481

SOMO: KUTUMIWA NA MUNGU (MCHUNGAJI KIONGOZI MKOA WA ARUSHA – MCH: JAMES NYANSIKA)

Mch. James Nyansika

Lazima ujiulize Mungu anatumia watu kufanya nini? Wewe kama wewe unasababisha nini katika jamii? Umeokoka kwa muda mrefu una miaka 15 katika wokovu, unasababisha nini katika ufalme wa Mungu?
Kumtumikia Mung sio kuwa na magonjwa, Mungu hauwezi kumtumikia wakati ukiwa na magonjwa, maana fedha na nguvu zako zote utazipeleka kwenye magonjwa badala ya kupeleka katika kumtumikia Mungu.
Lazima uelewe kusudi ni nini?
Uwepo wetu wa kuwa hapa tunaona Amani tele, furaha inazidi kila iitwapo leo, tunatumaini la milele kwa sababu kuna mtu ambaye alikubali kutumiwa na Mungu. Je wewe kama wewe umefanya nini katika ufalme wa Mungu kwaajili ya Mungu?
Mtu anaye tumiwa na Mungu
• Anajenga madhabahu ya Bwana
• Anasikia Neno kutoka kwa Bwana.
• Ana utayari kwaajili ya Bwana.
• Wanaotumiwa na Mungu sio waoga.
Mungu anaangalia moyo wa yule aliye karibu naye. Unaomba maombi ili upate hela ili iwe nini? Unaomba Mungu akupe mke mzuri ili iwe nini? Lazima uwe na sababu kwaajili ya Bwana.

(1 Samweli 16: 7 “ Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi “) Lakini Bwana akamwambia Samweli,
Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.

Je Mungu akiutazama moyo wako anaona nini? Kuna watu kazi yao ni kusengenya na kuwasema watumishi wa Mungu, wanamaneno mengi, wanazungumza mengi, sasa unakuta wana maombi hata ya kuwaumiza wengine sasa jiulize wewe mwenyewe je unatumiwa na nani wewe, unasababisha nini kwa wengine ambao Mungu amekupa kuwa nao?
Je unasababisha Amani? Upendo ni nini? Maana Mungu anatazamam moyo, Lazima ujipange kutumiwa na Bwana, wale wote walioko tayari kutumiwa an Bwana hawana hofu ya kuogopa kupambana na shetani maana shetani mwenyewe anatimua mbio kwa sababu anakazi na Bwana.

Anayetumiwa na Bwana hatishiwi na kitu chochote. Je moyo wako una nini wewe? Maana Bwana anatazama moyo ili akutumie, saa Bwana anakuangalai moyoni mwako anaona nini? Wacha maombi yako yakawe kwaajili yaw engine na sio masengenyo ili shetani asipate nafasi.
Unaposema Mchungaji kanikwaza au hajanifurahisha unaacha kazi ya Mungu sikiliza unatumiwa na Mungu sio Mchungaji.
Amua kumtumikia Bwana utaona matunda yake.

Karibu katika Ibada zetu,

Kanisa la Efatha Ministry Arusha lipo Kimandolu

Kwa msaada/maombi wasiliana na Mchungaji No 0767 103 231

NENO: KUTOKA MIKOANI – EFATHA MINISTRY MOROGORO

MTUMISHI RICKY MONGI.
SOMO: KUSHINDA MAMBO MAGUMU YANAYOTESA MAISHA YAKO.

Maisha ya watakatifu ni maisha ya mapambano maana adui (shetani ) hapendi kuwaona wakifanikiwa.
Wengine shetani amefanikisha kuwaweka katika vifungo na matatizo mbali mbali. Lakini cha ajabu ni kwamba walio wengi hupambana na tatizo siyo chanzo cha tatizo. Hii imewasababisha wao waendelee kuwa katika hivyo vifungo maana shina (chanzo) cha tatizo hakijashughulikiwa. YEREMIA 33:3 Inasema Mungu anasema tumuite ili atuonyeshe mambo makubwa na magumu. Mambo magumu yana tabia ya kujificha.


ZABURI 50:15 “ Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”
Siku ya mateso ni siku ya kumuita Mungu na siyo siku ya kujifungia ndani na kuanza kulia. Na tunamuita ili atuokoe, ni agizo katoa kwamba tumuite.


Kuna aina kuu tatu za maombi.
1. Maombi ya uhitaji. Hapa mtu anakuwa anaomba mahitaji yake kwa Mungu.
2. Maombi ya kubisha/kuita. Ndiyo haya Mungu anasema niite nami nitakuitikia.
3. Maombi ya kutafuta. Amesema katika MATHAYO 7:7
Siyo kila ombi linafaa kila mahali.


Sasa watu wengi wanateseka kwa sababu wanaangalia hayo mambo badala ya kumwangalia Yesu. Petro baada ya kutembea katika maji alivyoacha tu kumwangalia Yesu na kuangalia Upepo alianza kuzama, ndipo akaanza kumuita YESU amuokoe. Sasa jiulize ukiwa unapitia magumu huwa unamwita nani? Ukiangalia mazingira lazima ukwame.

Tatizo la watakatifu wengi wamechelewa kwa sababu wanaangalia mazingira na kumsikiliza shetani. Maana wakati wa magumu ndipo adui huwa anajitaidi kukusikilizisha habari zake. Kipindi cha magumu ndipo kipindi cha habari nyingi kutoka kwa shetani. Sasa utashinda kama una NENO ndani yako kama huna NENO huwezi kushinda.
1SAMWELI 17: 4-10 “ Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja.
Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba.
Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake. Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane”

Wana wa giza wana vitisho kwa sababu wameshindwa na hawana nguvu, pale utakapotishiwa na kuogopa ndipo adui atakapokufuata. Watakatifu badala ya kumwangali Yesu wanaangalia vitisho.
Wakati mwingine tunapita katika magumu ili Mungu adhihirike katika hayo magumu. Matatizo mengine huwa ni Fursa. Daudi aliona kumuua goliathi ni fursa lakini wana wa Israel waliona kuwa ni tatizo kwao.

Sikiliza utakapolitambua NENOla Mungu ndipo utakapo pata msaada katika vita vyako.

KUTOKA MIKOANI: SOMO “RUDI KATIKA NAFASI YAKO”

MTUMISHI: NOELY KAPINGA -EFATHA MINISTRY RUVUMA

Rudi katika nafasi yako ya utumishi. Ulikua msaada sana, ulitegemewa, kuna waliokuwa wanajifunza kwako.
Neno linasema;
(Waefeso 4;7)Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. “


Usimpe Ibilisi nafasi.


Sababu ibilisi anatafuta nafasi ili akutoe katika nafasi ,mfano Yuda Iskariote alimpa Ibilisi nafasi na shetani alimwingia (Luka 22:3),” Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.” ibilisi alipomuingia alifanikiwa kumtoa katika nafasi ya utume na uanafunzi wa Yesu, kama Ibilisi aliweza kumuingia Yuda aliyekua mwanafunzi wa Yesu, je? ataweza kukuacha wewe? hapo ni umakini unatakiwa, sababu ibilisi akikuingia anaua kila kitu na kukufanya uasi au usaliti, lakini Mungu ni wa huruma leo anataka kukurudisha kwenye nafasi.

(Ufunuo 2:4-5) “ Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, “
Ni lazima turudishe ule Upendo wetu wa kwanza .
Tusisingizie kazi, biblia inasema
Zaburi 104:23 “Mwanadamu anatoka na kazini na kwenye utumishi wake mpaka jioni”,
Nikushauri nenda kazini, ukitoka fanya majukumu ya utumishi wa Mungu, kama unatumika kanisani.
Mtumishi usielemee sehemu moja ni kazi na utumishi, (Zaburi 115:16) “Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.”
Rudi katika nafasi yako, wito wako .
Nakusihi angalia umeanguka wapi ?
Ukigundua hakikisha unafanya mambo mawili [2]


1.Tubu ; kutubu ni kubadilisha utu wa ndani ili ufanye mapenzi ya Mungu.
2.Ufanye kama mwanzo


Kumbuka wakati unaokoka ulikua na bidii, mtoaji, leo kuna utofauti. Mungu anataka ubadilike kwanza ndiyo akuinue, linaanza badiliko kisha Baraka zinafuata.
Mungu hakosei, naye anasema ataondoa kinara chako, utaona hasara kwenye biashara yako, ataondoa ile nuru katika biashara yako kwasababu umejua umekosa na haujataka kurudi kwenye nafasi yako.
Mungu ndiye kinara chako, ulikua mtoaji, leo huendi kanisani unasema michango mingi, biblia inatuambia
(1Wakorintho 16:1) ” Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.”
Tumeambiwa kuhusu habari ya changizo tuchange ipasavyo,

Utukufu wa Mungu unaoneka hata sasa – Ujenzi wa Kanisa kubwa unaoendelea kanisa la Efatha Kigoma mjini.

Hakika MUNGU wa Efatha ni MZURI sana, VIDEO inaonesha ujenzi wa Hema ya BWANA Ethatha Ministry Kigoma mjini. Ni baadhi tu ya MAMBO MAKUU anayotenda MUNGU ndani ya Huduma ya Efatha.

Huduma ya Efatha Kigoma chini ya Mchungaji Kiongozi BENSON MPELLE anawakaribisha watu wote katika Ibada mbalimbali zinazoendelea hapa kanisani.

RATIBA ZA IBADA NI KAMA IFUATAVYO

IBADA YA JUMPILI INAANZA: SAA 2:00 Asubuhi – 6:30 Mchana.

MAOMBI YA UPONYAJI NA UKOMBOZI JUMAMOSI: SAA 3:00 Asubuhi – 5:00 Asubuhi.

MADARASA YA WOKOVU NI JUMATATU NA ALHAMISI: SAA 10:00 Jioni – 12:00 Jioni.

Kwa msaada zaidi au ushauri wasiliana na Mchungaji kwa simu No:  0767 555 292

*** TAZAMA VIDEO YA UJENZI UNAOENDELEA EFATHA MINISTRY KIGOMA

 

Pichani CHINI: Mchungaji Kiongozi wa Efatha Ministry mkoa wa Kigoma na mkewe katika moja ya Ibada kanisani hapo.

 

Pichani CHINI: Kiongozi na mwanzilishi wa Huduma ya Efatha Duniani Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira (Katikati) akiwa na Mch. Kiongozi wa Efatha Ministry Kigoma pamoja na mkewe.

 

Pichani CHINI: Waimbaji wa mass choir Kigoma katika utumishi.