SOMO: NGUVU (MCH. CONSOLATA KITUNDU – WA HUDUMA YA EFATHA MKOA WA TANGA)

Mch. Consolatha Kitundu

Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,”
-Katika kutimiza malengo yako, zipo changamoto na maumivu ambayo utakutana, yatupasa kuvumilia na kuyastahimili maumivu utakayokutana nayo.
-Ili kutimiza malengo hayo ni lazima uwe na Nguvu ya Mungu itakayo kusababisha wewe kushinda katika kila changamoto utakazokutana nazo, maana shetani yupo ili kuzuia malengo yako yasitimie.
-Tambua kwamba unapopanga kuazimisha jambo lako, mfano biashara au kilimo, juwa wazi kuwa shetani nae anapanga kuharibu mipango yako ili usifanikiwe.
-Yatupasa kuwa na Nguvu ya Mungu kutimiza kila mpango katika maisha yetu.
-Yapo mambo ambayo shetani anaweza kuyatumia ili kuharibu mipango yako.
Roho ya kukata tamaa.
Waebrania 12:3 “Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.”
-Wakati upo katika kukamilisha malengo na mipango yako, shetani atakushambulia katika kila cheo la mipango yako ili akutakatishe tamaa.
-Ukikata tamaa huwezi kufanya jambo lolote.

Mithali 24:10 “Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.”
-Bila Nguvu ya Mungu ni lazima utazimia moyo,
Ili kukaa na Nguvu ya Mungu ni lazima ujue.
I. Baini umeitiwa nini.
II. Unafanya ulichoitiwa kwa usahihi.
III.Unafanya ulichoitiwa na Mungu kwa moyo WA kupenda.
IV. Unalijua Neno la Mungu.

UJUMBE: NEEMA – MCH. MICHAEL G. KUSWA (EFATHA MINISTRY MBEYA)

Warumi 8:14 “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. “

Kurithi kunakupa utoshelevu.palipo na Neema panakupa urithi na urithi unakupa kua mtoshelevu.

Palipo na Neema pana ufadhili, Ukiwa na Neema Mungu yupo ili kukufadhili.

2 Nyakati 17:3-5 “Naye Bwana alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye, asiyatafute mabaali;
4lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli. Kwa hiyo Bwana akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na Yuda wote; basi akawa na mali na heshima tele. ”

Neema inakupa kutenda ya Mungu .Neema itakupa kutenda yale ya Mungu. Palipo na Neema pana utoshelevu na utele.

2 Nyakati 1:7-10 “Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee Bwana Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye “

Roho wa kumcha Bwana atakusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.

2 Nyakati 9:22 “Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima. “

Palipo na Neema ya Mungu pana utukufu mwingi.Na mtu yoyote aliye na Neema amezungukwa na utukufu, Neema ikiwepo na Utukufu unakuwepo. Kama mtu ana Neema na utukufu umemzunguka..mtu huyu haishi kwa Imani bali anaishi kwa kuelewa. Neema inakutoa kunako Imani na unaanza kuishi kwa ufahamu na sio tena kwa imani maana utukufu wa Bwana umekuzunguka.

Kwenye Neema kuna kujibiwa maombi yako. Na kama eneo lina neeema basi maombi ya watu yatajibiwa.
Palipo na Neema maombi yanajibiwa kama Efatha tulivyo tuna Neema ndio maana maombi yetu yanajibiwa. Neema ipo ili kuimarisha na kuthibitisha maombi yako. Kwa hivyo unahitaji kuwa katika hali ya Neema ili maombi yetu yapate uthibitisho kwa Bwana.

Palipo na Neema pana ulinzi, ukiwa na Neema unalindwa. Neema ipo ili kukufanya wewe mtu wa Ibada na kukufanya wewe mtu wa ibada. Neeema inakupa kufanya ibada ya kumfurahisha Mungu, mpe Bwana Ibada iliyo kamili ili Bwana apate Kufurahishwa na Ibada ya moyo wako. Ukimfurahisha Mungu naye atakufurahisha.yoyote mwenye Neema anaaminiwa na Mungu; Mungu anakua na uamini wa kumpa mtu huyo mali.

Mtu mwenye Neema anakua kila iitwapo leo sio kiroho bali ni kimaendeleo, ukijichunguza na ukijua kua hakuna kitu kilichoongezeka hapo ujue kua Neema imepunguka kwako, Kile kitu kinachoweza kukusaidia icho kitakupa ongezeko. Neema inakupa kuongezeka, Mungu hamwamini kila mtu bali anamwamini mtu yule mwenye Neema tu.

Neema inamfanya Mungu akuamini na kukukabidhi mali zake ili uwe kituo cha ugawaji.

MWENE NEENA SIYO MCHOYO..

Mwenye Neema anahuruma ya Mungu na mtu huyu anahitaji sana roho ya shauri ili apate ushauri juu ya watu wa kuwahurumia.

Ukiwa na Neema Mungu anakufanya kua kituo cha ugawaji kwa wale ambao anakuelekeza au anakuambia juu ya habari ya ugawaji.

Neema inakupa kumcha Bwana ,utukufu wake unakuzunguka na ule ukuu wake unakua ulinzi kwako na familia yako.

PALIPO NA NEEMA PANA UVUMILIVU AU HESHIMA

MTU MWENYE NEEMA ANAHESHIMIKA.

MFANO : MSIBA WA MASIKINI WATU WANAO HUDHURIA NI WACHACHE SANA KULIKO WALE WANAOKUFA MATAJIRI …WANAOKUFA MATAJIRI MISIBA YAO INAFURIKA WATU KWASABABU TAJIRI HUYO AMESAIDIA WENGI.NA MSIBA WA TAJIRI HUYU KUNAKUA NA HESHIMA NA UNAONGELEWA VIZURI KWASABABU YA HELA ZA YULE TAJIRI .

UKIFA MASIKINI AU OMBA OMBA MSIBA WAKO UNAWEZA UHUDHURIWE NA WATU KUMI MAANA UNAKUFA NA HAUJAMSAIDIA MTU..PIA MSIBA HUU UTASEMWA KWA MENGI KWASABABU MTU HUYU AMEKUFA BILA HELA NA PIA HAKUNA ALYESAIDIWA NA MAREHEMU .

* UMASKINI NI MBAYA.

* UKIRI.BWANA YESU NAHITAJI HELA ILI NEEMA YAKO IKAE NAMIMI.

* UNAHITAJI NEEMA SANA .

MUNGU AKIKUPA NEEMA…NEEMA HIYO INAKUNEEMESWHA.

TUJIFUNZE KWA TAI NA TABIA ZAKE – (EFATHA MINISTRY USA RIVER)

Mchungaji: Baraka Lymo

Nguvu ya Mungu ipo kwaajili ya kufanya mambo makubwa. Kama unataka kufanya mambo makubwa basi leo mkono wa Bwana upo pamoja na wewe, Mkono wa Mungu uko na wewe saa hii

Waliokukataa mwaka huu lazima wakukubali, Kama ulifukiwa shimoni lazima ufukuliwe kutoka kwenye hilo shimo saa hii, Nipo mahali hapa kwenye madhabahu hii kukwambia kile Mungu anaenda kufanya kwako.

Mtu yeyete mwenye Nguvu za Mungu anafananishwa na Tai, mtu mwenye mawazo ya juu anafananishwa na tai. Tai Ni Ndege anaye ruka juu sana, Tai ana Kg 4 lakini anaweza akabeba mzigo wa kg 20 na akautoa mahali na kupeleka mbali, hivyo husijidharau kwa kuangalia mazingira yako.

Tai ana uwezo mkubwa wa kuona, anaweza akaona fursa ambazo wengine hawawezi kuona. Nguvu ya Mungu inakuja tu kwa wale walio na macho kama ya tai.

Tai anatabia ya kufundisha watoto wake na Tai mkubwa wa Efatha ni Josephat E. Mwingira, anatufundisha kila iitwapo leo

Je wewe ni tai? Mambie Mungu saa hii NAITAKA NGUVU YAKO siku ya leo.

KARIBU KANISANI EFATHA MINISTRY USA RIVER, KANISA LIPO LEGANGA USA RIVER ARUSHA WILAYA YA MERU, SHUKIA STAND YA POSTA, HALAFU FUATA NJIA HADI SHELI ILIYOKARIBU NA POSTA, KISHA KUNA NJIA NG’AMBO YA SHELI (YAANI UKIVUKA BARABARA), FUATA HIYO NJIA HADI MWISHO UTAKUTANA NA JENGO LETU MAHALI LILIPO…AU UKISHUKA LEGANGA, ULIZIA KANISA LA EFATHA MINISTRY LILILO JUU YA NDESAMBURO LODGE, UTAFIKISHWA…WOTE MNAKARIBISHWA…

Kwa Msaada zaidi wasiliana na Mchungaji kwa simu: 0763 480 481

SOMO: KUTUMIWA NA MUNGU (MCHUNGAJI KIONGOZI MKOA WA ARUSHA – MCH: JAMES NYANSIKA)

Mch. James Nyansika

Lazima ujiulize Mungu anatumia watu kufanya nini? Wewe kama wewe unasababisha nini katika jamii? Umeokoka kwa muda mrefu una miaka 15 katika wokovu, unasababisha nini katika ufalme wa Mungu?
Kumtumikia Mung sio kuwa na magonjwa, Mungu hauwezi kumtumikia wakati ukiwa na magonjwa, maana fedha na nguvu zako zote utazipeleka kwenye magonjwa badala ya kupeleka katika kumtumikia Mungu.
Lazima uelewe kusudi ni nini?
Uwepo wetu wa kuwa hapa tunaona Amani tele, furaha inazidi kila iitwapo leo, tunatumaini la milele kwa sababu kuna mtu ambaye alikubali kutumiwa na Mungu. Je wewe kama wewe umefanya nini katika ufalme wa Mungu kwaajili ya Mungu?
Mtu anaye tumiwa na Mungu
• Anajenga madhabahu ya Bwana
• Anasikia Neno kutoka kwa Bwana.
• Ana utayari kwaajili ya Bwana.
• Wanaotumiwa na Mungu sio waoga.
Mungu anaangalia moyo wa yule aliye karibu naye. Unaomba maombi ili upate hela ili iwe nini? Unaomba Mungu akupe mke mzuri ili iwe nini? Lazima uwe na sababu kwaajili ya Bwana.

(1 Samweli 16: 7 “ Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi “) Lakini Bwana akamwambia Samweli,
Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.

Je Mungu akiutazama moyo wako anaona nini? Kuna watu kazi yao ni kusengenya na kuwasema watumishi wa Mungu, wanamaneno mengi, wanazungumza mengi, sasa unakuta wana maombi hata ya kuwaumiza wengine sasa jiulize wewe mwenyewe je unatumiwa na nani wewe, unasababisha nini kwa wengine ambao Mungu amekupa kuwa nao?
Je unasababisha Amani? Upendo ni nini? Maana Mungu anatazamam moyo, Lazima ujipange kutumiwa na Bwana, wale wote walioko tayari kutumiwa an Bwana hawana hofu ya kuogopa kupambana na shetani maana shetani mwenyewe anatimua mbio kwa sababu anakazi na Bwana.

Anayetumiwa na Bwana hatishiwi na kitu chochote. Je moyo wako una nini wewe? Maana Bwana anatazama moyo ili akutumie, saa Bwana anakuangalai moyoni mwako anaona nini? Wacha maombi yako yakawe kwaajili yaw engine na sio masengenyo ili shetani asipate nafasi.
Unaposema Mchungaji kanikwaza au hajanifurahisha unaacha kazi ya Mungu sikiliza unatumiwa na Mungu sio Mchungaji.
Amua kumtumikia Bwana utaona matunda yake.

Karibu katika Ibada zetu,

Kanisa la Efatha Ministry Arusha lipo Kimandolu

Kwa msaada/maombi wasiliana na Mchungaji No 0767 103 231

HABARI KATIKA PICHA IBADA YA JUMAPILI JANUARI 14-2018 (EFATHA MINISTRY MWENGE, DSM)

PICHANI: Mchungaji Kiongozi Kanisa la mwenge Dar es salaam, Tanzania Mch. Aimana Dominick. Akimkaribisha Mnenaji katika Ibada ya leo, Mchungaji David Andulile Mwakisole (Mch. Kiongozi wa Efatha mkoa wa Kagera)

Mchungaji David Andulile Mwakisole aliye ongoza Ibada ya NENO hapa Efatha Ministry Kanisa la Mwenge Dar Es salaam Tanzania.

Waimbaji wa Efatha Ministry Mass Choir wakiongoza Ibada ya sifa na kuabudu hapa Efatha Ministry mwenge Dar Es salaam, Tanzania

PICHANI: Watumishi wa Mungu wakifuatilia Ibada ya Neno – Kanisani Efatha Ministry Mwenge Dar Es Salaam, Tanzania.

HERI YA MWAKA MPYA 2018 – TANGAZO

TANGAZO LA MWAKA 2018

Isaya 40:29-31 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; WATAPANDA JUU KWA MBAWA KAMA TAI; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”

Mwaka 2018 ni mwaka wa NGUVU , hutawahi kuzimia, hutawahi kushindwa hutawahi kuteswa, hutawahi kuwa dhaifu hutawahi kulala kwa sababu ya maradhi. NGUVU ya Mungu kutoka Mbinguni itakujia na kukutia NGUVU na kukupa kushinda.
Yale yote uliyoshindwa kufanya miaka iliyopita sasa utaenda kuyafanya kwa ushindi, ingawa unaonekana ni dhaifu lakini itatoka nguvu ndani yako na kushinda kila kizuizi kilichopo mbele yako, kamwe hutashindwa tena.

Mwaka huu utakwenda kufanya uharibifu katika kambi ya ibilisi, atalia ili kutafuta usaidizi na kamwe hataweza kupata, kilio na majonzi vitatawala katika kambi yake, popote utakapo tokeza kama kuna uchawi wowote kutakuwa na mpasuko na uharibifu mkubwa. Kama kuna mchawi au mganga wa kienyeji katika familia yako mwaka huu ni mwaka wa kuzika. Yeyote aliyekuwa anakuzuia kung’aa kamwe hataweza tena, mwaka huu ni mwaka wako kwa sababu ni mwaka wa NGUVU hivyo ushindi ni wako.

Watu wengi watatamani kukusogelea ili wainuliwe kwa sababu wewe utakuwa umeinuliwa, wakati wote kuanzia sasa hadi milele hutakuwa pekeyako kwa sababu utukufu wa Mungu utakuja katika maisha yako ili kusababisha NGUVU kuja kwako.
Kuhangaika na kung’ang’ania kumekwisha.

SEMINA YA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU, EFATHA MINISTRY MWENGE DAR ES SALAAM,

 

MCHUNGAJI: VICKY TEMU.

AHADI za MUNGU ni KWELI, Mungu akisema jambo HABADILIKI, akisema NITAKUBARIKI jua kuwa ATAKUBARIKI, akisema atakupa AFYA NJEMA hakuna ATAKAYE IZUILIA, akisema hutakufa kwa magonjwa ndivyo itakavyokuwa. Mungu hajawahi kuwa muongo, AHADI ZAKE ni KWELI.

Mungu alimbariki Ibrahimu kwa Baraka za kila aina, ndipo Ibrahimu akamuuliza Mungu je! Baraka hizi zote atazimiliki mjakazi wangu? Ndipo Mungu akamwambia kuwa atakaye miliki Baraka zake ni mwanaye atakaye toka katika viuno vyake. Mungu akamwambia Ibrahimu kuwa  uzao wake utakuwa kama nyota za angani, baada ya Mungu kumuahidi Ibrahimu kuwa atampa mtoto, ilipita miaka mingi sana; lakini Mungu alitimiza kile ambacho alimuahidi  Ibrahimu.

Ahadi za Mungu kwako ni Amina; na zitatimia haijalishi itapita miaka mingapi.

Kutoka 23:20-27 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali. Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande. Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. ”

Mungu amemtuma malaika mbele yako ili kukufikisha kule ambapo amekuandalia, kuna mahali ambapo Mungu amekuandalia palipo na Baraka zako, unapaswa kumsikiliza malaika aliyetumwa mbele yako.  Malaika tayari ameanza safari na wewe, hivyo unapaswa kuwa makini kwa jinsi unavyo enenda mbele zake usije ukamtia kasilani maana hata kusamehe.

Unaweza kumkasilishaje? Kwa tabia zako, malaika aliyeko mbele yako ni mtakatifu, hivyo na wewe unapaswa kutembea katika Utakatifu ili muweze kwenda pamoja. Amosi 3:3 “Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” huyo malaika kama utakuwa na tabia nje ya Utakatifu hamuwezi kupatana wala kutembea pamoja. Ili uweze kufika kule ambapo Mungu amekukusudia yakupasa ubadilike na kuishi maisha Matakatifu.

Huyo  malaika aliyeko mbele yako unapaswa kumsikiliza maana anamaelekezo ya ile njia uiendeayo. Unapo isikiliza sauti yake na kutenda yale Mungu ananena kupitia ile sauti ndipo Mungu atakuwa adui wa aui zako.

Yamkini ulikuwa unateswa na magonjwa, watu walikutendea uadui ambao huujui, ukishatembea vizuri na kusikiliza sauti yake, Mungu atakuwa adui wa adui zako na atakuwa mtesi wa hao wanao kutesa.

Wewe utanyamaza lakini yeye atapigana na wanao pigana nawe.

Kutoka 23:25 “Nanyi MTAMTUMIKIA Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.” kusudi kubwa tulilo itiwa huku duniani ni KUMTUMIKIA MUNGU.  Je! Wewe unamtumikia Mungu?

Kumtumikia Mungu haina maana kuwa lazima usimame madhabahuni na kuhubiri, la! Bali hata pale ulipo; ukisimama vizuri kwenye nafasi yako yeyote ile uliyopewa, wewe ni MTUMISHI wa Bwana. Hata ukiwa Baba au mama wa familia pia ni nafasi ambayo umepewa, hivyo unapaswa kuitumikia hiyo nafasi kwa uaminifu, kwa sababu ukitumika kwa uaminifu yeye anasema kuwa “atabariki chakula chako na maji yako naye atakuondolea magonjwa ndani yako”.

Kila Ahadi ya Mungu inamaagizo yake; Mara nyingi tumechelewesha Ahadi za Mungu kutimia katika maisha yetu kwa sababu ya kuto kufanya kwa bidii maagizo tuliyopewa, na kuto kusikiliza sauti ya Bwana.

Mungu hajawahi kushindwa na kitu chochote, ukiona Ahadi zako zinachelewa shida si Mungu bali ni wewe mwenyewe. Mungu akisema anasubiri ukifanye kile ambacho amesema, ukisimama kwenye nafasi yako na yeye atasimama kwenye nafasi yake ili kukubariki. Kumbukumbu 28:1 “Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;”  

Zaburi 62:11 “Mara moja amenena Mungu; Mara mbili nimeyasikia haya, Ya kuwa nguvu zina Mungu,” Kama Mungu ndiye mwenye NGUVU, je! ni kitu gani kinashindikana kwake? Mungu ndiye aliyeumba Mbingu na nchi, na vyote vipo katika UWEZA WAKE, chochote unacho kihitaji kiko kwake. Mara nyingi tumetumainia nguvu zetu, za wanadamu au za dunia hii lakini hazijatusaidia kwa chochote.

 Mfano:- Mtu anaweza akawa anaumwa, akaenda Hospitalini na kuambiwa kuwa ugonjwa alionao hauwezi kupona, anapo rudi nyumbani anakaa na kusema kuwa anasubiria kufa tu! huu ni upumbavu.  Unapaswa kumtafuta yule aliye kuumba, YEYE anayejua mateso yako yote anajua kila kiungo chako. Mkimbilie YEYE ana NGUVU na UWEZO wa KUKUPONYA.

Mungu ni mwenye NGUVU hajawahi KUSHINDWA na chochote, shida ni kwetu sisi wanadamu maana tunamashaka na YEYE, Mtu anaweza kumwamini Daktari na si Mungu.

MUNGU ANA NGUVU NA UWEZA WOTE MWAMINI YEYE TU ATAKUWEZESHA.

 

MCH. ANDREW SWAI – IBADA NOV 26 – 2017

SOMO: ACHA DHAMBI UKAISHI.

Ezekiel 18:21-23 “Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?”

Ukaache njia zako mbaya leo na ukamgeukie Bwana, kughairi inamaana kuwa ni kugeuka na kuacha njia zako mbaya, ukifanya hivyo utaishi, kuishi maana yake ni nini? Hutakuwa na maradhi wala magonjwa.
Chukia dhambi na kuamua kuziacha, amua kutafakari sheria za Mungu kila wakati, ukiacha njia mbaya atakusamehe, nawe utaishi. Unahitaji kuishi, Mungu hafurahii mtu kufa katika dhambi, amua leo kuwa inatosha kutenda dhambi na uamue kumgeukia Mungu ili ukaishi, dhambi ndizo zinakuletea magonjwa na kifo.

Bwana Yesu anakupenda na anataka leo upokee uponyaji wako na uhai mpya ili kwamba ukaishi, baada ya Mungu kutaka kuiangamiza Ninawi watu wa mahali pale walipoamua kuacha dhambi na kumgeukia Mungu, ndipo Mungu alipo ghairi kuuangamiza. Amua kufanya mapenzi ya Mungu ili uishi na uwe mbali na magonjwa na mateso.

MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA – IBADA NOV 26 – 2017

Zaburi 103:3 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, ” Mungu akikusamehe anakuponya na magonjwa yako yote, leo ni siku ya kusamehewa na kuondolewa magonjwa.

Zaburi 103:8 ” Bwana amejaa HURUMA na NEEMA, Haoni HASIRA upesi, ni mwingi wa FADHILI. ” Baba yetu wa Mbinguni ni wa HURUMA na NEEMA, na kwa sababu ya HURUMA na NEEMA zake ameizuia hasira yake isituangamize kwa sababu ya dhambi na uovu wetu, Mungu aliye Baba yetu anatupenda na kwa sababu hiyo amekwisha kutusamehe.

Fungua moyo wako na usiangalie yale yanayo kutesa, maana Mungu anaweza kukuponya ameizuia hasira yeke isiwake juu yako ili akuponye leo.

Mungu anapo samehe dhambi zetu anatuponya na yale yanayo tutesa.