UJUMBE: FURAHA YA BWANA (MCH. MICHAEL G. KUSWA) EFATHA MINISTRY MBEYA

Mchungaji Kiongozi mkoa wa Mbeya, Mch. Michael G. Kuswa

Furaha ya Bwana ni UPAKO, na hii huja kama huna chuki (HILA) ndani yako.

Jiumbie furaha ndani yako, wala mtu asiondoe kicheko chako wala mtu asiondoe furaha ndani yako.

Na kama ukiwa na furaha hata ndoa yako itakua nzuri kwasababu mume wako au mke anafuraha.

Hauwezi kugombana na watu kama unafuraha, Furaha inakupa kuvumilia, pale panapo ugomvi furaha hii inakupa kunyamaza.

Ukitembea na furaha, furaha hii inatatawanyika. Kwa mabinti furaha hii inakupa kuvuta au kuvutia yule mtu husika.. sio kwa kujikoboa kwako ila hutokana na furaha yako.

Usipokua na furaha ataununue perfume ya bei ghali vipi, hautanukia vizuri kwasababu hauna furaha ila kwa mwenye furaha itanukia vizuri.

Furaha inakupa changamko, na wale wafanyao kazi ofisini si kwasababu ya ubora wao ila ni kwasababu ya ile furaha yako.

Furaha ni tabia ya Mungu .

Kama huna ulinzi basi hautakua na furaha.
Unapokosa ulinzi na unapokosa iyo furaha hapo hakuna wokovu.
Furaha ni jambo la muhimu sana katika maisha yako.

Ni wenye furaha tu wawezao kufanya ukombozi.
Furaha ya Bwana inatupa nguvu na inatufanya tufanye kazi katika ukamilifu. Sio kazi ya Bwana tu bali ni kazi zote,

Furaha ya Bwana inakupa utulivu, Haikupi kukurupuka. Ukiwa na Furaha hukurupuki hata siku moja.

Furaha ya Bwana inakupa stamina ya kiroho.

Mateso sio mtu ila ni roho
Furaha itaondoa uadui wa ile zawadi uiyoletewa,Furaha itakupa kupambanua.

Furaha haikuruhusu kuwaza kinyume na kweli.

Furaha inakupa hali ya utulivu na utulivu unaleta ujasiri.

Ukiruhusu furaha kua kwako unaruhusu kuvutia.
Ukiruhusu furaha kwa njia ya upendo utabarikiwa.
Ukiwa na furaha Mungu anakufanya kua kituo cha ugawaji.

Furaha inakupa kufanya kwa moyo.Mtu huyu hatumiki kwaajili yake mwenyewe ila anatumika kwaajili ya mwengine.
Kufanya kazi kwa Moyo si kwasababu ya maisha yako.
Kujifunza kuna kupa maisha marefu.

Fikia mahali unafanya kazi kwa moyo si kwasababu yako bali ni kwaajli ya
wengine.

Kufanya kazi kwa moyo kutadhihirisha kua wewe unajitambua wewe ni nani.

Ukianza kufanya kazi kwa Moyo Mungu anakuthibitisha kisha anakupa kujitambua.

Mithali 3:4

Kufanya kazi kwa moyo kuna kupa kuishi kwa burudani.

Kile unachokitoa kwaajili ya mwengine huo ndio uzuri wako.

Ukiona hufanyi kazi kwa moyo inamaana una uchawi ndani yako.

Huzuni inakupeleka panapo uasi.

Katika furaha ndiko kunakupa kuvumilia mabaya.

FURAHA NI HALI YA NDANI.

 

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – NOV 26 – 2017

Leo ni siku yako ya kubadilishwa;

Siku zote Mungu anaiangalia siku, kwa sababu yeye hayuko katika wakati wala majira, Mungu ni Mungu na matendo yake yanaelekezwa kwa siku, wewe ndio unaye tazamia wakati na majira lakini ndani yake hakuna majira, Yeye ni yule yule jana leo na hata milele.
Hii inamaana gani? Inamaana jinsi alivyokuwa jana ndivyo hivyo hivyo alivyo leo, na kama alivyo leo ndivyo atakavyokuwa kesho, Mungu wetu habadiliki, wewe unaweza kubadilika lakini Yeye kamwe hata badilika. Wewe unaweza kubadilika na unatakiwa kubadilishwa ili kwamba uweze kutembea pamoja naye na ili uwe tayari kwa ajili yake.
Yeye yupo tayari kwa ajili yako, Je! Wewe uko tayari kwa ajili yake?

Mathayo 14:22-27 “Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. ….. ”
Yesu akawaambi wanafunzi wake nendeni mbele kule ambako aliwaagiza waende, lakini katikati ya safari YESU akatokea kutoka kule mlimani alikokuwa akiomba peke yake. Siku unapotaka kuomba mbele za Mungu haijalishi ni watu wangapi wamekaa kando yako unapaswa kuwa peke yako, Mungu anapenda watu ambao wako peke yao. Wasahau wale walio kando yako na ujitazame wewe mwenyewe. Usimwangalie mume/mke wako, au ndugu yako aliye kaa jirani yako bali jiangalie mwenyewe na utamwona Mungu leo.

Yesu alitoka kule Mlimani akiwa tayari KUDHIHIRISHA NGUVU za MUNGU, huwezi kupata NGUVU za MUNGU mpaka uwe Mlimani na ukiwa peke yako. Tamani uwe peke yako ukiwa mbele za Mungu.
Baada ya maombi yale Yesu akatoka akiwa na UDHIHIRISHO wa NGUVU za MUNGU, unapotoka Mlimani unakuwa na uhakika wa NGUVU za MUNGU. Baada ya Yesu kufika kwa wanafunzi wake “akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Siku ya leo ninakwambia kuwa USIOGOPE maana kuna kitu kitakutokea katika maisha yako, jiandae kupokea muujiza wako.

2Wafalme 4:18-37 “Hata yule mtoto alipokua, ikawa siku moja alitoka kwenda kwa baba yake kwenye wavunao. Akamwambia baba yake, Kichwa changu! Kichwa changu! Naye akamwambia mtumishi wake, Mchukue kwa mama yake. Akamchukua, akampeleka kwa mama yake, naye akakaa magotini mwake hata adhuhuri, kisha akafa………..”

Watu wengi hapa Duniani wako katika mazingira haya inawezekena ukawa ni wewe, huyu mwanamke mshunami ambaye mtoto wake alikufa, alijitambu hivyo akasema kuwa hahitaji kulia. Alijua kuwa mtoto alitoka kwa Mungu hivyo akajua kuwa Mungu anaweza kufanya jambo kwa ajili ya mtoto wake.
Yule mtoto alikuwa amekufa lakini yule mwanamke alikataa kulia na kukubaliana na ile hali ya kifo cha mtoto wake, alijua wapi pa kwenda maana alijua kuwa mtoto alitoka kwa Mungu. Ndipo alipochukua punda na mjakazi na kumwambia kuwa afanye haraka ili kuwahi kwa Mtumishi wa Mungu. Unapotaka kitu kitokee kwako fanya haraka kuwahi kwenye uwepo wa Mungu, maana Mungu wetu si mvivu hivyo unapaswa kufanya haraka ukitaka kitu kutoka kwake.

 

USHUHUDA WA FAMILIA YA MAMA MARY MWANKANYE

Tunamshukuru sana Mungu kwa mambo aliyo tutendea, tunamshukuru kwa kuweza kumchukua Mama yetu akiwa ameokoka na alikuwa akimtumikia Mungu mpaka mwisho wa maisha yake. Tuna washukuru wana Efatha kwa upendo wenu mkuu mliouonyesha kwa kipindi chote.

Sisi kama familia tumemuona Mungu wa Efatha kupitia Mama yetu, pamoja na changamoto alizopitia hakurudi nyuma wakati wote alimtumainia Mungu mpaka mwisho wa maisha yake. Tunamshukuru sana Mungu kwa ajili ya Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mama Eliakunda Mwingira, kwa kuweza kututia moyo kwa kipindi kigumu tulichopitia. Tunamshukuru sana Mungu kwa Neema aliyompa Mtume na Nabii kwa kuweza kutunza Kanisa Vyema, nasi tunaamini kuwa siku moja tutaungana nae na kuabudu pamoja na Wana Efatha.

NENO: KUTOKA MIKOANI – EFATHA MINISTRY MOROGORO

MTUMISHI RICKY MONGI.
SOMO: KUSHINDA MAMBO MAGUMU YANAYOTESA MAISHA YAKO.

Maisha ya watakatifu ni maisha ya mapambano maana adui (shetani ) hapendi kuwaona wakifanikiwa.
Wengine shetani amefanikisha kuwaweka katika vifungo na matatizo mbali mbali. Lakini cha ajabu ni kwamba walio wengi hupambana na tatizo siyo chanzo cha tatizo. Hii imewasababisha wao waendelee kuwa katika hivyo vifungo maana shina (chanzo) cha tatizo hakijashughulikiwa. YEREMIA 33:3 Inasema Mungu anasema tumuite ili atuonyeshe mambo makubwa na magumu. Mambo magumu yana tabia ya kujificha.


ZABURI 50:15 “ Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”
Siku ya mateso ni siku ya kumuita Mungu na siyo siku ya kujifungia ndani na kuanza kulia. Na tunamuita ili atuokoe, ni agizo katoa kwamba tumuite.


Kuna aina kuu tatu za maombi.
1. Maombi ya uhitaji. Hapa mtu anakuwa anaomba mahitaji yake kwa Mungu.
2. Maombi ya kubisha/kuita. Ndiyo haya Mungu anasema niite nami nitakuitikia.
3. Maombi ya kutafuta. Amesema katika MATHAYO 7:7
Siyo kila ombi linafaa kila mahali.


Sasa watu wengi wanateseka kwa sababu wanaangalia hayo mambo badala ya kumwangalia Yesu. Petro baada ya kutembea katika maji alivyoacha tu kumwangalia Yesu na kuangalia Upepo alianza kuzama, ndipo akaanza kumuita YESU amuokoe. Sasa jiulize ukiwa unapitia magumu huwa unamwita nani? Ukiangalia mazingira lazima ukwame.

Tatizo la watakatifu wengi wamechelewa kwa sababu wanaangalia mazingira na kumsikiliza shetani. Maana wakati wa magumu ndipo adui huwa anajitaidi kukusikilizisha habari zake. Kipindi cha magumu ndipo kipindi cha habari nyingi kutoka kwa shetani. Sasa utashinda kama una NENO ndani yako kama huna NENO huwezi kushinda.
1SAMWELI 17: 4-10 “ Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja.
Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba.
Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake. Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane”

Wana wa giza wana vitisho kwa sababu wameshindwa na hawana nguvu, pale utakapotishiwa na kuogopa ndipo adui atakapokufuata. Watakatifu badala ya kumwangali Yesu wanaangalia vitisho.
Wakati mwingine tunapita katika magumu ili Mungu adhihirike katika hayo magumu. Matatizo mengine huwa ni Fursa. Daudi aliona kumuua goliathi ni fursa lakini wana wa Israel waliona kuwa ni tatizo kwao.

Sikiliza utakapolitambua NENOla Mungu ndipo utakapo pata msaada katika vita vyako.

SOMO: WEWE NI NANI NA MUNGU AMEWEKA NINI NDANI YAKO.

PASTOR CHARLES KARIUKI-KENYA

Mwanzo 1: 26 -28 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba……”

Tatizo kubwa tulilonalo huku Duniani, ni watu kutokujitambua. Kama hujitambui huwezi kujua una nini au uwezo wako wa kutenda ni upi. Kuna baadhi ya watu wana amini kile ambacho ma-babu zao waliwaambia, na wengine wana amini kile ambacho waalimu wao Waliwaambia, na kwa sababu waliwaambia madhaifu mengi sana kuhusu wao na hivyo ndivyo wanavyojichukulia.

Mungu alipo mtokea Gideoni na kumwambia wewe ni mtu shujaa, Mungu alijua kuwa Gideoni ni shujaa lakini Gideoni mwenyewe alikuwa anajiona tofauti. Gideoni alijiona dhaifu kwani alikuwa anajificha mbele ya jeshi la Wamidiani. Gideoni aka anza kujielezea kuwa familia yake ilikuwa ni maskini na yeye pia alikuwa maskini hivyo akakataa kuambiwa kuwa ni shujaa.

Mungu kamwe habadilishi kile ambacho alikinena, na hayuko tayari kubadilisha kile ambacho amekinena. Unapaswa kubadilisha akili yako, kwa sababu Mungu habadiliki kamwe. Kile ambacho MUNGU anakijua kuhusu wewe ni kweli, tofauti na kile ambacho unakijua kuhusu wewe ambacho maranyingi e ni uongo.
Mungu alimwambia Gideoni kuwa ana nguvu ya kuokoa taifa na si familia yake tu. Pale alipokuwa anajificha si mahali pake, yeye ni mkuu hivyo achukue nafasi yake ili afikie ukuu wake.

Mungu alipo muumba mwanadamu alimbariki, ili akawe na mamlaka ya kutawala kila eneo la nchi maana ndiyo milki yake. Mamlaka yako haipo tu kwenye nyumba yako, bali hata katika anga lako na kitu chochote kile kilicho katika nchi kipo katika milki yako.

Hapa duniani Mungu aliukabidhi wajibu wa kumiliki au kutawala kwa wanadamu, na alipotoa hiyo mamlaka Mungu akaacha kufanya kazi. Si kwamba Mungu alichoka bali ni kwa sababu kazi yake aliikabidhi kwa mwanadamu.
Mungu wetu si Mungu wa kuchanganya mambo kwa sababu yeye ni Mungu wa mipangilio na anapo kukabidhi kitu wewe, hawezi kuja kukuingilia anakupa uhuru kamili katika kitu hicho.

Sisi ni watawala, hivyo Mungu alipo muumba mwanadamu ilibidi amjaribishe kwanza kama uumbaji wake upo kwa huyo mwanadamu. Hivyo Mungu aliwaumba wanyama na kumletea Adamu ili awapatie majina. Mungu alipo ona kuwa Adamu ndani yake kuna uumbaji baada ya kuwapa majina wanyama wote, akajua kuwa pia kuna Utawala ndani ya Adamu. Na ndio maana hata baada ya Mungu kumuumba mwanamke alimpa Adamu ili ampe jina.

Mwanzo 2:4-8 “Hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi…… ”

Ardhi ilikuwepo lakini Mungu hakuweka kitu chochote kile mpaka alipomuumba Mwanadamu kwa sababu hakukuwa na kitu kinachoweza kuilima ardhi ndipo Mungu akamuumba mwanadamu ili aweze kuilima ardhi.

Mungu hawezi kuruhusu uzalishaji utokee pale ambapo hakuna mzalishaji, jukumu moja ambalo Mungu alimpa mwanadamu ni kusimamia rasilimali zake hapa Duniani. Mungu anavutiwa na wasimamizi, ukimuonyesha Mungu kuwa wewe ni msimamizi basi ataruhusu Baraka zake kwako lakini ukimuonyesha kuwa si msimamizi kamwe hataruhusu Baraka zake kwako kwa sababu atakuwa na uhakika kuwa hutaweza kuzisimamia.

Mfano: Unapanga chumba baada ya miezi sita umechafua nyumba ya watu haijulikani hata rangi, halafu unasema eti kwa sababu unalipia, usipokuwa mwaminifu kwa vya watu Mungu hawezi kukupa vya kwako.

Simamia vizuri kile kidogo ambacho ulichonacho ili Mungu aweze kukuongezea kingine kikubwa zaidi.

Zaburi 115:16 “Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.”
Hapa Duniani ni kwetu maana tumepewa na Mungu na wala hatuhami haraka maana Mbinguni ni kwake hapa ni kwetu, simamia rasilimali zako vizuri ili Mungu azidi kukubariki .

BREAKING NEWS!

Mtumishi wa Mungu Dr Morris Cerullo amewasili nchi Tanzania alasiri ya leo, na kufikia katika Hotel ya Kimataifa ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro, ambapo kesho siku ya Jumamosi anatarajiwa kufika na kuhubiri katika Kusanyiko Kuu la tisa la wana  Efatha linaloendelea hapa Precious Center Kibaha Tanzania.

Ni heshima kubwa kwa Tanzania naEfatha  kupokea ugeni huu muhimu, najua Tanzania haitabaki kama ilivyokua. KARIBU SANA TANZANIA MTUMISHI WA MUNGU ALIYE HAI DR. MORRIS CERULLO, KARIBU SANA EFATHA MINISTRY.

Watu wote wanaopenda kufika mahali hapa mnakaribishwa sana, tunawapenda sana wageni wetu, walete wagonjwa na wenye uhitaji mbalimbali Mungu atawaponya na kuwafungua.

KATIKA PICHA: Mtumishi wa Mungu Dr.  Morris Cerullo wa Huduma kubwa ya Morris Cerullo World Evangelism  akiwasili katika Hotel ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro, ambapo amepokelewa na wenyeji wake Efatha Ministry.

SOMO: KUSHUGHULIKIA ROHO ZA KUCHELEWESHA – KUSANYIKO LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA

ASKOFU MARK KARIUKI – NAIROBI KENYA:

Imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa Neno kutoka kwa Baba. Jinsi unavyopokea Neno la Mungu maisha yako yanabadilika na wewe inabidi upokee hilo Neno ili libadilishe maisha yako. Mungu hashughuliki na watu kama kundi bali kama mtu binafsi maana anakuletea mahitaji yako kama mtu binafsi.
Mwanzo 21:1-2” Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema. Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu”.

Mungu atakutembelea wiki hii kama alivyomtembelea Sara na kufanya kama alivyoahidi kwako. Mafanikio ni lazima siyo uchaguzi kwa sababu Mungu aliumba watu ili kuzaa na kuongezeka akimaanisha mafanikio. Kama hakuna kuzaa kuna nguvu inayo kuzuia kufanikiwa, hizo nguvu zina masikio na zinasubiri useme na ukisema zinatii unachosema maana Mungu anakaa ndani yako, hivyo ukisema zinasikia. Tumia kinywa chako kujitabiria kile ambacho unataka Mungu akutendee na kitatimia kwako.

Maisha ni mapambano na haya mapambano ni ya kila siku kama Paulo alivyosema katika Efeso 6: 11”Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.
Vita vyetu siyo katika damu na nyama, bali katika Roho.
Silaha za vita vyetu siyo katika mwili bali katika roho. Kama kuna vita ina maana kuna adui hata kama unamjua ama hujui.

Yohana 10: 10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”.
Mwizi huja, siyo wewe unaenda kumtafuta bali yeye anakuja siyo kwamba unapenda au hupendi ,Petro anasema muwe timamu na muwe imara maana shetani anazunguka zunguka akimtafuta mtu ammeze. Hivyo shetani humtafuti ila yeye anakutafuta na anakuja kwako ili kuiba, Kuua na Kuharibu.

Na atakuja kwako wakati wowote, hivyo ni muhimu usimpuuze mwizi, usichukulie kana kwamba hakuna mwizi bali ujue yupo na ni adui, na ni janga kumpuuza mwizi. Ukitambua kuna mwizi kabla hajakamilisha lengo lake, basi utakuwa umeshafanya jambo la kumfanya ashindwe kukuibia. Ukishamgundua mwizi kabla hajaiba atakukimbia, lakini usipomtambua atakusumbua, kukunyanyasa na kukutesa.
Hivyo mtambue mwizi ili asikuibie.

Kuna mambo unayaangalia na unagundua kwamba hukuyakamilisha na ni kwa sababu yupo mwizi aliyekuibia.
Hosea 4:6” Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”

Miradi uliyoianza hukuanza ili usiikamilishe ila mwizi au kwa jina jingine mcheleweshaji amekufanya usikamilishe. Inabidi ujue nini kimeibiwa kwako, labla ni afya, maono, ndoto, mafanikio yako yamecheleweshwa, kama mwizi yupo huwezi kwenda mahali. Kuna nguvu inatumika, mafuta yanatumika, tairi linalika lakini gari halisongi mbele, unatembea lakini husongi mbele uko pale pale. Hicho kilicho chelewesha ndoa, nyumba, watoto, cheo ama furaha yako lazima kishughulikiwe leo.
Hasira ya kiungu ukujilie, hasira hii ilimjia Yesu na ilipomjilia aliingia hekaluni mwenyewe pasipo usaidizi na akapindua pindua meza. Hasira hii ikikujia hakuna mchawi atakaa kwenye mazingira yako.

USHUHUDA : NENO LA MUNGU LINABADILISA MAMBO – KUNA FAIDA KATIKA KUSIKIA NENO KUTOKA MADHABAHUNI

Suma William

Naitwa Suma William, napenda kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyo nitendea, nilikuja Efatha mwaka 2008, wakati huo sikua na sehemu ya kulala hata nguo ya kuvaa ilikuwa shida. Namshukuru Mungu mwaka 2009 kwenye Kusanyiko kuu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira Alisema kuna watu wataenda kujenga nyumba, kuwa na Makampuni na magari, nililishika lile neno na sasa Mungu amebadilisha maisha yangu sana, amenipa vitu hivyo vitatu ambavyo vilitamkwa, Mungu amenipa nyumba nzuri, gari na Kampuni. Namshukuru sana kwa matendo makuu aliyonitendea .

Karibu na wewe ambaye hujafika bado hapa Precious Center Kibaha ili USIKIE NENO lako ambalo litabadilisha maisha yako.

USHUHUDA: MCH. AGNESS AKISIMULIA ALIYOTENDEWA NA MUNGU WA EFATHA, FUATILIA.

Mchungaji Agness Ndunguru

Naitwa Mchungaji AGNES L. NDUNGURU, mwaka 2009 mume wangu RICHARD NDUNGURU alipata neema ya kuwafundisha watu wa Trenet tv, wakati huo ndio kusanyiko lilikuwa limeanza lakini yeye alinikaribisha siku ya mwisho ya kusanyiko na hapo ndipo ilikuwa chanzo cha wokovu wangu.

Kusanyiko la mwaka 2010 ambalo lilikuwa kusanyiko langu la kwanza baada ya kuokoka. Nilimtumia dada yangu nauli akaja kwenye kusanyiko. Dada yangu alikuwa na ujauzito kwa miaka mitano na kila mahali alikuwa anatembea na begi akitarajia kujifungua. Alipofika hapa siku ya ufunguzi wa Kusanyiko alianza kutapika kwa muda wa siku tatu, na ule ujauzito ukapotea akapokea uponyaji wake, tumbo lote likaisha na akawa mzima kabisa.

Mume wangu alikua hajapandishwa cheo muda mrefu kwenye kusanyiko la mwaka 2012 nikanunua picha ya Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na sasa amepandishwa cheo mara mbili.

Namshukuru sana Mungu kwa matendo makuu aliyonitendea mimi na familia yangu.

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA PILI KUSANYIKO KUU LA TISA LINALOENDELEA PRECIOUS CENTER KIBAHA

Baadhi ya picha za matukio mbalimbali yanayoendelea hapa katika mji wa Bwana Preciou center Kibaha Tanzania, wewe ambaye hujafika hakikisha unafika ili upokee Baraka, uponyaji, kufunguliwa pamoja mafundisho ya NENO la MUNGU ambayo yatabadilisha maisha yako. ACHA KUTESEKA NJOO UKUTANE NA MKONO WA MUNGU.

PICHANI CHINI: Waimbaji wa Efatha Mass choir kutoka nchini Zambia wakimsifu MUNGU kupitia uimbaji katika kusanyiko la tisa linaloendelea hapa Precious center Kibaha Tanzania. MUNGU awabariki kwa uimbaji mzuri.

 

PICHANI CHINI: Watumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Mitume na Wachungaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania, wakiwa Ukumbini Precious center kibaha katika kusanyiko la tisa linaloendelea.

 

 

PICHANI CHINI: Waimbaji wa Efatha Mass choir kutoka mwenge Dar es salaam wakimtumikia MUNGU kwa uimbaji katika Kusanyiko la tisa linaloendelea hapa Precious Center Kibaha Tanzania.