HABARI PICHA KUSANYIKO KUU LA TISA (SIKU YA NNE).

Baadhi ya picha kutoka Kusanyiko Kuu 2017 hapa Precious center Kibaha Tanzania, kama bado hujafika amua leo uje kabla kusanyiko hili halijaisha. MUNGU yupo hapa.

PICHANI : Waimbaji wa Efatha Mass choir wakimsifu Mungu katika Kusanyiko kuu la tisa linaloendelea hapa Precious Center Kibaha.

PICHANI CHINI: Mama Eliakunda Mwingira akiingia ndani ya Ukumbi wa Precious Center Kibaha, tayari kwa Ibada.

PICHANI CHINI: Watumishi mbalimbali wakifuatilia Ibada katika Ukumbi mkubwa na wakisasa PRECIOUS CENTER Kibaha Tanzania.

PICHANI CHINI: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira pamoja na mtangulizi wa Mtumishi wa Mungu Dr Morris Cerullo hapa Precious Center Kibaha.

 

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA TATU KUSANYIKO KUU LA TISA 2017 – PRECIOUS CENTER KIBAHA

Ikiwa ni siku ya tatu ya Kusanyiko Kuu la tisa la wana Efatha linaloendelea katika ukumbi mkubwa na wa aina yake wa PRECIOUS CENTER uliopo hapa KIBAHA kwa Mathias, tunakuletea baadhi tu ya picha mbalimbali, Kumbuka bado hujachelewa kwani Kusanyiko hili litafungwa siku ya Jumapili usiku, Karibu sana Mpendwa najua lipo jambo ambalo Mungu amekuandalia hivyo usipange kukosa.

PICHANI CHINI: Waimbaji wa Efatha Ministry Mass choir wakimtumikia MUNGU kwa uimbaji kwenye kusanyiko kuu hapa Precious center Kibaha Tanzania.

 

PICHANI CHINI: ASKOFU JOSEPH KAZHILA Akfundisha NENO la MUNGU juu ya IMANI

 

PICHANI CHINI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Watumishi wengine wakifuatilia Ibada.

 

PICHANI CHINI: Watumishi wa MUNGU wakiwa katika Ibada ya maombi inayoendelea hapa Precious center Kibaha Tanzania.

 

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA PILI KUSANYIKO KUU LA TISA LINALOENDELEA PRECIOUS CENTER KIBAHA

Baadhi ya picha za matukio mbalimbali yanayoendelea hapa katika mji wa Bwana Preciou center Kibaha Tanzania, wewe ambaye hujafika hakikisha unafika ili upokee Baraka, uponyaji, kufunguliwa pamoja mafundisho ya NENO la MUNGU ambayo yatabadilisha maisha yako. ACHA KUTESEKA NJOO UKUTANE NA MKONO WA MUNGU.

PICHANI CHINI: Waimbaji wa Efatha Mass choir kutoka nchini Zambia wakimsifu MUNGU kupitia uimbaji katika kusanyiko la tisa linaloendelea hapa Precious center Kibaha Tanzania. MUNGU awabariki kwa uimbaji mzuri.

 

PICHANI CHINI: Watumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Mitume na Wachungaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania, wakiwa Ukumbini Precious center kibaha katika kusanyiko la tisa linaloendelea.

 

 

PICHANI CHINI: Waimbaji wa Efatha Mass choir kutoka mwenge Dar es salaam wakimtumikia MUNGU kwa uimbaji katika Kusanyiko la tisa linaloendelea hapa Precious Center Kibaha Tanzania.