USHUHUDA WA FAMILIA YA MAMA MARY MWANKANYE

Tunamshukuru sana Mungu kwa mambo aliyo tutendea, tunamshukuru kwa kuweza kumchukua Mama yetu akiwa ameokoka na alikuwa akimtumikia Mungu mpaka mwisho wa maisha yake. Tuna washukuru wana Efatha kwa upendo wenu mkuu mliouonyesha kwa kipindi chote.

Sisi kama familia tumemuona Mungu wa Efatha kupitia Mama yetu, pamoja na changamoto alizopitia hakurudi nyuma wakati wote alimtumainia Mungu mpaka mwisho wa maisha yake. Tunamshukuru sana Mungu kwa ajili ya Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mama Eliakunda Mwingira, kwa kuweza kututia moyo kwa kipindi kigumu tulichopitia. Tunamshukuru sana Mungu kwa Neema aliyompa Mtume na Nabii kwa kuweza kutunza Kanisa Vyema, nasi tunaamini kuwa siku moja tutaungana nae na kuabudu pamoja na Wana Efatha.

USHUHUDA: JUMAPILI HII..

Naitwa Catherine Agustino napenda kumshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyo nitendea. Namshukuru Mungu kwa uzima na afya aliyo nipa, nilipata ugonjwa wa ganzi kwa muda wa miaka saba, ganzi hiyo ilinivaa kuanzia miguuni mpaka kifuani nilihangaika sana Hospitalini na hata kwa waganga wa kienyeji ili kutafuta uponyaji lakini sikupata.

Wakati huo nilikuwa sijaokoka na nilikuwa sitaki kabisa kusikia habari za kuokoka, mtu akiniambia kuwa Yesu ananipenda nina muuliza huyo Yesu aliniona wapi?. Siku moja jirani yangu alinikaribisha kwake ili niangalie TRENET TV, ndipo nilipomuona Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiimba na kucheza pamoja na Efatha Mass Choir, nilivutiwa sana na ile Choir na jinsi Mtumishi wa Mungu alivyokuwa anacheza.

Jumapili iliyofuata nilipata Neema ya kuja Kanisani na nikapokea Uponyaji wangu na ndipo nikaamua kumpa Bwana Yesu maisha yangu. Nina mshukuru sana Mungu kwani baada ya kuokoka, mwanangu amepata watu wa kumsomesha na sasa anasoma Efatha Seminary. Sina cha kumpa Mungu zaidi ya kumrudishia YEYE SIFA na UTUKUFU maana ANASTAHILI.

USHUHUDA: MTUMISHI ALINIBARIKI NIKA CHAGULIWA KUWA DIWANI, NA MENGINE MUNGU KANITENDEA.

MH. DAVID BOCHELA

Mweshimiwa David Bochela {sisimizi}, Namshukuru sana Mungu kwa matendo makuu anayonitendea kwani kila kitu kizuri nilicho nacho nimekipata Efatha. Mwaka 2013, Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, alinibariki akaniambia nitafika pale ambapo Mungu amenikusudia kufika.

Akaniuliza umri wangu, aliponiuliza nikajua anamaana kubwa kwangu, nilipomjibu akaniambia utafika . Akaniagiza nimpende sana Mungu na niwaheshimu watu ndipo nitafika mbali.

Namshukuru Mungu amenibariki, nilinunua shamba kubwa Dodoma, pia mwaka 2015 niligombea udiwani na nikashinda. Mwaka huu Bwana ameniinua tena, nimepata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji Dodoma. Ninamshukuru Mungu wa Efatha kwa kunitoa kutoka katika hali ya kukata tama mpaka kuja kuitwa mweshimiwa, ni kwa neema yake.

USHUHUDA: AMEONANA NA MWANAE BAADA YA KUPOTEZANA KWA MUDA MREFU

PIENSIA MAPUNDA

Naitwa Piensia Mapunda. Namshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu kwangu. Ndani ya miaka 15 niliishi mbali na mtoto wangu, na sikujua alipokuwa, kwa sababu hakukuwa na mawasiliano kati yangu na yeye.

Siku moja akanipigia simu akaniambia kuwa anahali mbaya sana, lakini hakuniambia alikuwa wapi. Baadae nilikuja kufahamu kwamba alikuwa Tanga. Namshukuru Mungu, Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema mwaka huu ni mwaka wa kujibiwa maombi, nilipofika kule Tanga, nilimkuta amekuwa mvuta bangi na mlevi wala haeleweki. Nilifanikiwa kumleta Efatha na baada ya kumleta hapa amebadilika kwani amempokea Yesu

USHUHUDA: AMEPONYWA HIV ALIPOKUJA KUSANYIKO LA MWAKA 2016

HESHIMA JOHN

Naitwa Heshima John. Napenda kumshukuru Mungu kwa matendo yake ya ajabu kwangu. Ilikuwa mwaka 2016 nilivimba tumbo nikaenda kupima nikaambiwa nina ugonjwa wa Ini na HIV. Ndipo nikaja kwenye kusanyiko kuu la mwaka 2016, Baba Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akawaombea wagonjwa na mimi nikiwa mmoja wao.

Baada ya kuombewa, nikakurudi katika eneo langu la kulala, nilishangaa nikaanza kulia mwenyewe, na baadae nikaanza kucheka pasipo kujua kilichokuwa kinanichekesha, kuanzia hapo tumbo langu likaanza kuuma na nilikojoa sana na kutapika. Tumbo likaisha lote na niliporudi nyumbani nikaenda kupima haukuonekana ugonjwa wowote ule. Napenda kumshukuru sana Mungu kwa matendo yake ya ajabu kwangu, Sifa na Utukufu anastahili yeye peke yake. Sina cha zaidi cha kumpa zaidi ya kumshukuru Mungu wangu.

USHUHUDA: MUNGU AMENIPONYA UGONJWA WA AJABU

Grace Kauma Dar – Shalom

Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniponya. Niliteseka kwa muda wa miaka miwili nikiwa naumwa tumbo sana. Nilipokwenda Hospitali nilifanyiwa Ultrasound na haikuoyesha kitu chochote. Madaktari wakaamua kunifanyia upasuaji. Baada ya ule upasuaji nikakaa miaka mitatu siwezi kufanya kitu chochote kile, ile hali ya kutokufanya kazi ilikuwa inanitesa sana.

Nilipokuwa nikilala usiku nikawa nakula nyama, na nikiamka asubuhi siwezi kula kitu chochote zaidi ya kunywa pepsi mbili asubuhi, mchana na usiku, kwa siku nilikuwa na kunywa soda sita . Baada ya kuhangaika sana hadi kwa waganga ili nipone lakini sikupata uponyaji .

Wakati nilipokuwa ninahangaika, Daktari alisema kuwa tatizo langu halieleweki na nisitegemee kuolewa, labda baada ya miaka 15 au 20, ndipo naweza kuolewa. Napenda kumshukuru Mungu nilipokuja Efatha, katika Kusanyiko la mwaka 2013 nilipokea uponyaji nikawa mzima.

Katika Kusanyiko la mwaka 2014 nilikuwa Mbeya Baba Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akatangaza “ watu wengi wanaenda kuoa na kuolewa” na mimi nilikuwa namsikiliza nikiwa Mkoani Mbeya, nikasema na mimi ni mmoja wao.

Tarehe 10/7/2015 nilifunga ndoa katika Madhabahu ya Efatha, namshukuru sana Mungu kwani ameondoa aibu yangu na ibilisi ameshindwa. Nawashauri ndugu zangu msisisikilize kile ambacho watu au Madaktari wana waambia kuwa haiwezekani, bali mwangalieni Mungu kwani anaweza yote.

USHUHUDA: NIMEPONYWA, MAPEPO YALIYOKUA TUMBONI MADAKTARI WALISEMA NI UJAUZITO SASA YAMETOKA NIMEPONA

ESTER MUSA – DSM

Kwa muda wa mwaka mmoja nilikuwa nahisi tumboni kuna kitu kinatembea na nilipokwenda Hospitali nikaambiwa kuwa mimi ni mjamzito japo nilikuwa naona siku zangu kama kawaida.

Nilikuwa naingia kwenye siku zangu kwa siku tano lakini baada ya hali hii nikawa napata hedhi kwa siku mbili na damu ikawa ni kidogo sana. Nilipokuja katika Kusanyiko hili linaloendelea Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akasema kuwa “kuna mtu anahisi kama ana mtoto tumboni lakini huyo si mtoto bali ni pepo kuanzia saa hii uwe huru kwa Jina la Yesu”.

Mtu huyo alikuwa ni mimi nikapokea uponyaji saa ile ile. Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniponya katika Kusanyiko hili, nimeuona mkono wake hata kabla kusanyiko halijaisha..

USHUHUDA: MUNGU AMETUPA MUUJIZA WA MTOTO, MADAKTARI WALISEMA HATU

Mr na Mrs Nili David

Mr na Mrs Nili David, kutoka Arusha. Tunamshuhukuru Mungu kwa kututendea maajabu,mimi na mke wangu tulikaa katika ndoa yetu kwa muda wa miaka mitatu pasipo kupata mtoto.

Tulipokwenda Hospitali Daktari akatuambia kuwa magroup yetu ya damu hayaendani hivyo hatuwezi kupata mtoto. Lakini mwaka jana kwenye Kusanyiko Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akasema kuwa, kuna watu ambao hawana watoto na Daktari amewaambia hawatapata watoto kutokana na magroup yao ya damu kuwa tofauti, lakini mwakani watakuja na watoto wao hapa huku wakishangilia.

Mimi na mke wangu tulilipokea lile Neno na kuendelea kumkumbusha Mungu kila siku, mwezi uliofuata baada ya Kusanyiko, Mungu akatusikia akalitimiza Neno la Mtumishi wake. Leo tumekuja na mtoto katika madhabahu hii, tukimshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyotutendea.

USHUHUDA: NILIKUA NIMEPOOZA SASA NIMEPONA NILIPOKUJA KUSANYIKO LA 2016

BAHATI JACKSON

Naitwa Bahati Jackson. Namshukuru Mungu kwa kuniponya ugonjwa wa kupooza viungo vya mwili. Mwaka 2016 nilipooza viungo vya mwili wangu kwa muda wa miezi sita. Nikiwa katika hali hiyo nilikuja katika Kusanyiko lililofanyika mwaka huo na ndipo nilipokutana na mkono wa Mungu aliyeniponya.

Pia kupitia Kusanyiko Mungu ameniinua kiuchumi kwani nimeweza kumalizia nyumba yangu na kufungua duka la vipodozi. Namshukuru sana Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kwa kuniombea, sasa mimi ni mzima kabisa

USHUHUDA: NIMEPONYWA TATIZO LA KUPOOZA KWENYE KUSANYIKO LA MWAKA 2016.

GLORY SAID

Glory Said, Namshukuru Mungu kwa kuniponya kwani nilikuwa naumwa ugonjwa wa kupooza kwa muda wa miaka mitatu. Kwa muda wote huo sikuweza kufanya chochote kile, nilikuwa siwezi kula mwenyewe mpaka nilishwe, siwezi kuvaa nguo mwenyewe na hata kuoga.

Nilipoletwa hapa kwenye Kusanyiko la mwaka jana 2016 Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema wagonjwa wote waliokuja watarudi wakiwa wamepona, nililipokea lile Neno na baada ya maombezi nilipokea uponyaji wangu. Namshukuru sana Mungu kwa kuniponya kwani nilikuwa siwezi kufanya kazi yoyote, lakini sasa naweza kufanya kazi zangu zote.