KUSAUJUMBE KUSANYIKO KUU LA TISA EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA SIKU YA MWISHO.

Mtume na Nabii: Josephat Elias Mwingira

Huwezi kusimama kinyume na ibilisi bila NGUVU ya Mungu. Unaweza kuona watu waliokoka kama ni watu waliopoteza muelekeo, ambao wamejaa na matatizo na mahangaiko ya kila aina, lakini hiyo si kweli, ukweli wa mambo ni kuwa watu waliiokoka ni washindi. Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. ”

1Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. ”
Wokovu ni Neema inayokupelekea wewe kuwa na Nguvu ya Mungu, hivyo unapo pata wokovu ambao tunapata kupitia Pendo la Mungu inakuwa ni rahisi kwako kufurahia Neema ya Mungu.
Bwana Yesu alisema tangu siku za Yohana Mbatizaji mpaka siku ya unyakuo ni wale tu wenye Nguvu ya Mungu ndio watakaoweza kuuridhi Ufalme wa Mungu.
Huwezi kuuridhi Ufalme wa Mungu au kula mema ya Mungu kama huna Nguvu zake. Huwezi kufurahia wema wa Mungu kama huna Nguvu zake, utaishia kuona watu wengine wakifanikiwa, wakiwa na magari na nyumba nzuri. Watu waliookoka si kwamba wanamtumikia Mungu ili waende Mbinguni tu bali wanafanya hivyo kwa sababu wanamfurahia Mungu wao, hivyo wanakuwa na Nguvu ya Mungu ya kuwawezesha kufanikiwa sana.

Zaburi 23:5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.”

Hii inamaana kuwa ulimwengu umetawaliwa na uovu na wana wa uovu tu ndio watakao fanikiwa, hivyo kwa wewe ili uweze kufurahia Dunia hii unahitaji kuwa na Nguvu ya Mungu. Watu wa Mungu wanahitaji kuwa na U-ungu ndani yao ili waweze kuifurahia hii Dunia ya Mungu.

Shetani ni muongo, mwizi na muuaji na hawezi kuruhusu uwe na maisha mazuri kwa urahisi kwa sababu anajua kuwa kama ataruhusu wewe kustawi utasababisha Ufalme wa Mungu kusonga mbele.

Luka 4:5-6 “Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. ”

Katika uwepo wa Nguvu za Mungu kuna kuinuliwa na kupandishwa na kutukuzwa.
Kumbukumbu 28:13 “Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. ”
Mtu yeyote mwenye Nguvu za Mungu, anakuwa kichwa na si mkia, muda wote anakuwa juu na sio chini. Mtu mwenye Nguvu za Mungu haimizwi kushika maagizo au amri za Mungu.

Comments

comments

Comments are closed.