KUTOKA MIKOANI: SOMO “RUDI KATIKA NAFASI YAKO”

MTUMISHI: NOELY KAPINGA -EFATHA MINISTRY RUVUMA

Rudi katika nafasi yako ya utumishi. Ulikua msaada sana, ulitegemewa, kuna waliokuwa wanajifunza kwako.
Neno linasema;
(Waefeso 4;7)Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. “


Usimpe Ibilisi nafasi.


Sababu ibilisi anatafuta nafasi ili akutoe katika nafasi ,mfano Yuda Iskariote alimpa Ibilisi nafasi na shetani alimwingia (Luka 22:3),” Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.” ibilisi alipomuingia alifanikiwa kumtoa katika nafasi ya utume na uanafunzi wa Yesu, kama Ibilisi aliweza kumuingia Yuda aliyekua mwanafunzi wa Yesu, je? ataweza kukuacha wewe? hapo ni umakini unatakiwa, sababu ibilisi akikuingia anaua kila kitu na kukufanya uasi au usaliti, lakini Mungu ni wa huruma leo anataka kukurudisha kwenye nafasi.

(Ufunuo 2:4-5) “ Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, “
Ni lazima turudishe ule Upendo wetu wa kwanza .
Tusisingizie kazi, biblia inasema
Zaburi 104:23 “Mwanadamu anatoka na kazini na kwenye utumishi wake mpaka jioni”,
Nikushauri nenda kazini, ukitoka fanya majukumu ya utumishi wa Mungu, kama unatumika kanisani.
Mtumishi usielemee sehemu moja ni kazi na utumishi, (Zaburi 115:16) “Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.”
Rudi katika nafasi yako, wito wako .
Nakusihi angalia umeanguka wapi ?
Ukigundua hakikisha unafanya mambo mawili [2]


1.Tubu ; kutubu ni kubadilisha utu wa ndani ili ufanye mapenzi ya Mungu.
2.Ufanye kama mwanzo


Kumbuka wakati unaokoka ulikua na bidii, mtoaji, leo kuna utofauti. Mungu anataka ubadilike kwanza ndiyo akuinue, linaanza badiliko kisha Baraka zinafuata.
Mungu hakosei, naye anasema ataondoa kinara chako, utaona hasara kwenye biashara yako, ataondoa ile nuru katika biashara yako kwasababu umejua umekosa na haujataka kurudi kwenye nafasi yako.
Mungu ndiye kinara chako, ulikua mtoaji, leo huendi kanisani unasema michango mingi, biblia inatuambia
(1Wakorintho 16:1) ” Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.”
Tumeambiwa kuhusu habari ya changizo tuchange ipasavyo,

Comments

comments

Comments are closed.