MAOMBI : MKESHA MAALUM WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.

MKESHA WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA:

1Wakorintho 2:4-5 “Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.” Paulo alipokuwa akihubiri akiomba hekima ya Mungu isimame, alikuwa anatamani kataika kuhubiri kwake kusiwe katika Hekima ya kibinadamu bali katika Nguvu za Roho Mtakatifu.

Imani ni njia pekee ya kupokea kutoka kwa Mungu, imani inatupa uwezo wa kupokea vitu kutoka kwa Mungu maana pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu ila tukiwa na imani tunaweza kupokea vitu kutoka kwa Mungu.

Ombi: Muombe Mungu aruhusu Roho wake aje kwako ili akuumbie imani uweze kupokea vitu kutoka kwake.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *