NENO: IBADA YA JUMAPILI NOVEMBA 5 – 2017

NENO LA MUNGU IBADA YA TATU: EFATHA MINISTRY MWENGE DAR ES SALAAM.
MCHUNGAJI ANJELINA MDADILA.
Neno la Mungu ni kweli; Usiwe msikiaji wa NENO tu bali uwe mtendaji pia, ukitendea kazi kile ambacho umesikia utaona mabadiliko katika maisha yako.
 
Kwa nini huu ni mwaka wa kujibiwa maombi, je! Hapo mwanzo Mungu alikuwa hajibu maombi yetu? La! Mungu anajibu maombi kila saa na kila wakati, lakini alicho kusudia mwaka huu ni kujibu maombi yetu kwa UKUU wake. Hakikisha unaishi maisha MATAKATIFU ndipo huu mpango wa KUJIBIWA MAOMBI utafanikiwa kwako.
 
Kutoka 3:9 “Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; “ Mungu alichoka kuona maumivu na mateso ya watoto wake, mapenzi ya Mungu ni kuona watoto wake wakiwa huru na wenye furaha pia. Mungu aliwatoa wana wa Israel ili waende kumtumikia yeye. Mungu anapo kuokoa ni ili ukamtumikie YEYE, usiokoke kwa sababu unataka kuponywa magonjwa, hayo si makusidio ya Mungu kukuokoa bali makusudio yake ni wewe umtumikie yeye, atakapoona kuwa unamtumikia ndipo ataponya magonjwa yako nawe utakuwa huru.
 
Mungu mapenzi yake ni wewe uwe katika hali nzuri na si uwe kwenye maumivu, maana anataka umwabudu kwa furaha na shangwe.
 
Umejihukumu sana jisamehe na uwasamehe wengine maana kwa kadri unavyo endelea kukumbuka yale machungu na maumivu yaliyopita unajichelewesha kupokea mambo mapya, jifunze kujisamehe na kusamehe wengine. Acha kujikumbushia yaliyopita Mungu anasema anapo samehe hakumbuki tena. Waebrania 10: 7-18 “Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi. ”
 
Waebrania 10:12-17 “Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. ” Bwana Yesu alikufa mara moja ili tusamehewe, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona, alifanyikika sadaka ili mimi na wewe tuokolewe na kupona, hivyo ugonjwa au udhaifu wowote ule usikusumbue maana Bwana Yesu alilipia pale msalabani.
 
YESU ANAKUPENDA SANA.. Wewe ambaye hujaokoka wakati uliokubalika ni sasa, chukia maisha ya dhambi unayoishi kila siku,, amua sasa na YESU ATAKUSAIDIA

Comments

comments

Comments are closed.