NENO: KUTOKA MIKOANI – EFATHA MINISTRY MOROGORO

MTUMISHI RICKY MONGI.
SOMO: KUSHINDA MAMBO MAGUMU YANAYOTESA MAISHA YAKO.

Maisha ya watakatifu ni maisha ya mapambano maana adui (shetani ) hapendi kuwaona wakifanikiwa.
Wengine shetani amefanikisha kuwaweka katika vifungo na matatizo mbali mbali. Lakini cha ajabu ni kwamba walio wengi hupambana na tatizo siyo chanzo cha tatizo. Hii imewasababisha wao waendelee kuwa katika hivyo vifungo maana shina (chanzo) cha tatizo hakijashughulikiwa. YEREMIA 33:3 Inasema Mungu anasema tumuite ili atuonyeshe mambo makubwa na magumu. Mambo magumu yana tabia ya kujificha.


ZABURI 50:15 “ Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”
Siku ya mateso ni siku ya kumuita Mungu na siyo siku ya kujifungia ndani na kuanza kulia. Na tunamuita ili atuokoe, ni agizo katoa kwamba tumuite.


Kuna aina kuu tatu za maombi.
1. Maombi ya uhitaji. Hapa mtu anakuwa anaomba mahitaji yake kwa Mungu.
2. Maombi ya kubisha/kuita. Ndiyo haya Mungu anasema niite nami nitakuitikia.
3. Maombi ya kutafuta. Amesema katika MATHAYO 7:7
Siyo kila ombi linafaa kila mahali.


Sasa watu wengi wanateseka kwa sababu wanaangalia hayo mambo badala ya kumwangalia Yesu. Petro baada ya kutembea katika maji alivyoacha tu kumwangalia Yesu na kuangalia Upepo alianza kuzama, ndipo akaanza kumuita YESU amuokoe. Sasa jiulize ukiwa unapitia magumu huwa unamwita nani? Ukiangalia mazingira lazima ukwame.

Tatizo la watakatifu wengi wamechelewa kwa sababu wanaangalia mazingira na kumsikiliza shetani. Maana wakati wa magumu ndipo adui huwa anajitaidi kukusikilizisha habari zake. Kipindi cha magumu ndipo kipindi cha habari nyingi kutoka kwa shetani. Sasa utashinda kama una NENO ndani yako kama huna NENO huwezi kushinda.
1SAMWELI 17: 4-10 “ Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja.
Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba.
Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake. Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane”

Wana wa giza wana vitisho kwa sababu wameshindwa na hawana nguvu, pale utakapotishiwa na kuogopa ndipo adui atakapokufuata. Watakatifu badala ya kumwangali Yesu wanaangalia vitisho.
Wakati mwingine tunapita katika magumu ili Mungu adhihirike katika hayo magumu. Matatizo mengine huwa ni Fursa. Daudi aliona kumuua goliathi ni fursa lakini wana wa Israel waliona kuwa ni tatizo kwao.

Sikiliza utakapolitambua NENOla Mungu ndipo utakapo pata msaada katika vita vyako.

Comments

comments

Comments are closed.