NENO: MKESHA MAALUM WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU

Na Mtume na Nabii: Josephat Elias Mwingira.

Huu ni mwaka wa nne wa Mtembeo wa Mungu, huu si Mtembeo wa Mwanadamu bali ni wa Mungu kutembea na watu wake wale ambao amewaridhia, hivyo basi huu ni mwaka wa udhihirisho wa Nguvu za Mungu; hutakaa utikiswe na chochote, shetani hatakaa akutishie tena kwa sababu una Nguvu za Mungu.

Matendo 1:8 “Lakini mtapokea NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa MASHAHIDI wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Hii ni Ahadi ya Mungu kwa wale wanao mwamini Yesu Kristo, kama wewe ni mmoja waio Ahadi hii ni yako si ya shangazi yako wala mjomba wako.
Wewe unaye mwamini unapewa Ahadi hii ili uwe shahidi wa mambo ya Mungu kupitia Kristo Yesu; hivyo ukiipata NGUVU hiyo unakuwa na uwezo wa kujionyesha wewe ni muwakilishi wa Mungu huku duniani.

Nguvu za Roho Mtakatifu zinapokuja kwetu, tunafaidiaka na nini.?
1. Katika uwepo wake Roho Mtakatifu utajua mambo ya sasa na yale yajayo. Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” Ukiijua kweli ya Mungu ndiyo itakufanya uishi, Bwana Yesu akasema huyo Roho atakapokuja atawaingiza katika kweli; kwa nini katika kweli? Kwa sababu ndiyo itakayo kupa kuishi.

2. Utajua kuwa una Baba Mwana na Roho Mtakatifu,
3. Utayajua yale mambo ambayo umekirimiwa na BABA wa Mbinguni. 1Wakorinto 2:12 “Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.” Mungu kila iitwapo leo anajambo la kipekee kwa ajili yetu lakini sisi hatujui na ndiyo maana tunakufa maskini.
4. Roho huyu anapokuja kwako anakupa UJASIRI wa kulinena NENO la Mungu. Matendo 5:12 “Na kwa mikono ya Mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;” Roho anapokuja NGUVU ya kuponya inadhihirika.

Nguvu za Roho Mtakatifu zinapokuja kwetu, tunafaidiaka na nini.?
• Roho huyu anapokuja anafanya kanisa liongezeke na kusababisha injili kuenea kwa kasi.
Matendo 6:7 “Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.”
• Uwepo wa Roho Mtakatifu unasababisha Karama na Vipawa vya Roho Mtakatifu kutenda kazi ndani yetu.
1 Wakorinto 12:28-31 “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii?…..”
• Uwepo wake humimina Pendo la Mungu kwa wale waaminio, wakati Roho wa Mungu anapokuja, anakuja na Pendo la Mungu na hukufanya wewe uwe mtendaji wa mambo ya Mungu, kwa sababu bila Pendo huwezi kuwa mkweli. 1Yohana 4:6-7 “Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu……..”

• Roho huyu anapokuja anatupa uhakika wa Wokovu wetu. 1 Yohana 5:12 “Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.” Yeye anapokuja anamleta Roho wa Kristo ndani yako na anakuhakikishia uzima wa milele, tunamuhitaji Roho Mtakatifu ili atupe Nguvu ya umilele.
• Roho huyu hukusaidia kupata vitu kutoka kwa Mungu, hukusaidia kunena kwa lugha, pia itakusaidia kutoa vitu kwenye ulimwengu wa Roho na kuvileta katika ulimwengu wa damu na nyama.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *