Posts

NENO: KUTOKA MIKOANI – EFATHA MINISTRY MOROGORO

MTUMISHI RICKY MONGI.
SOMO: KUSHINDA MAMBO MAGUMU YANAYOTESA MAISHA YAKO.

Maisha ya watakatifu ni maisha ya mapambano maana adui (shetani ) hapendi kuwaona wakifanikiwa.
Wengine shetani amefanikisha kuwaweka katika vifungo na matatizo mbali mbali. Lakini cha ajabu ni kwamba walio wengi hupambana na tatizo siyo chanzo cha tatizo. Hii imewasababisha wao waendelee kuwa katika hivyo vifungo maana shina (chanzo) cha tatizo hakijashughulikiwa. YEREMIA 33:3 Inasema Mungu anasema tumuite ili atuonyeshe mambo makubwa na magumu. Mambo magumu yana tabia ya kujificha.


ZABURI 50:15 “ Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”
Siku ya mateso ni siku ya kumuita Mungu na siyo siku ya kujifungia ndani na kuanza kulia. Na tunamuita ili atuokoe, ni agizo katoa kwamba tumuite.


Kuna aina kuu tatu za maombi.
1. Maombi ya uhitaji. Hapa mtu anakuwa anaomba mahitaji yake kwa Mungu.
2. Maombi ya kubisha/kuita. Ndiyo haya Mungu anasema niite nami nitakuitikia.
3. Maombi ya kutafuta. Amesema katika MATHAYO 7:7
Siyo kila ombi linafaa kila mahali.


Sasa watu wengi wanateseka kwa sababu wanaangalia hayo mambo badala ya kumwangalia Yesu. Petro baada ya kutembea katika maji alivyoacha tu kumwangalia Yesu na kuangalia Upepo alianza kuzama, ndipo akaanza kumuita YESU amuokoe. Sasa jiulize ukiwa unapitia magumu huwa unamwita nani? Ukiangalia mazingira lazima ukwame.

Tatizo la watakatifu wengi wamechelewa kwa sababu wanaangalia mazingira na kumsikiliza shetani. Maana wakati wa magumu ndipo adui huwa anajitaidi kukusikilizisha habari zake. Kipindi cha magumu ndipo kipindi cha habari nyingi kutoka kwa shetani. Sasa utashinda kama una NENO ndani yako kama huna NENO huwezi kushinda.
1SAMWELI 17: 4-10 “ Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja.
Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba.
Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake. Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane”

Wana wa giza wana vitisho kwa sababu wameshindwa na hawana nguvu, pale utakapotishiwa na kuogopa ndipo adui atakapokufuata. Watakatifu badala ya kumwangali Yesu wanaangalia vitisho.
Wakati mwingine tunapita katika magumu ili Mungu adhihirike katika hayo magumu. Matatizo mengine huwa ni Fursa. Daudi aliona kumuua goliathi ni fursa lakini wana wa Israel waliona kuwa ni tatizo kwao.

Sikiliza utakapolitambua NENOla Mungu ndipo utakapo pata msaada katika vita vyako.

KUTOKA MIKOANI: SOMO “RUDI KATIKA NAFASI YAKO”

MTUMISHI: NOELY KAPINGA -EFATHA MINISTRY RUVUMA

Rudi katika nafasi yako ya utumishi. Ulikua msaada sana, ulitegemewa, kuna waliokuwa wanajifunza kwako.
Neno linasema;
(Waefeso 4;7)Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. “


Usimpe Ibilisi nafasi.


Sababu ibilisi anatafuta nafasi ili akutoe katika nafasi ,mfano Yuda Iskariote alimpa Ibilisi nafasi na shetani alimwingia (Luka 22:3),” Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.” ibilisi alipomuingia alifanikiwa kumtoa katika nafasi ya utume na uanafunzi wa Yesu, kama Ibilisi aliweza kumuingia Yuda aliyekua mwanafunzi wa Yesu, je? ataweza kukuacha wewe? hapo ni umakini unatakiwa, sababu ibilisi akikuingia anaua kila kitu na kukufanya uasi au usaliti, lakini Mungu ni wa huruma leo anataka kukurudisha kwenye nafasi.

(Ufunuo 2:4-5) “ Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, “
Ni lazima turudishe ule Upendo wetu wa kwanza .
Tusisingizie kazi, biblia inasema
Zaburi 104:23 “Mwanadamu anatoka na kazini na kwenye utumishi wake mpaka jioni”,
Nikushauri nenda kazini, ukitoka fanya majukumu ya utumishi wa Mungu, kama unatumika kanisani.
Mtumishi usielemee sehemu moja ni kazi na utumishi, (Zaburi 115:16) “Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.”
Rudi katika nafasi yako, wito wako .
Nakusihi angalia umeanguka wapi ?
Ukigundua hakikisha unafanya mambo mawili [2]


1.Tubu ; kutubu ni kubadilisha utu wa ndani ili ufanye mapenzi ya Mungu.
2.Ufanye kama mwanzo


Kumbuka wakati unaokoka ulikua na bidii, mtoaji, leo kuna utofauti. Mungu anataka ubadilike kwanza ndiyo akuinue, linaanza badiliko kisha Baraka zinafuata.
Mungu hakosei, naye anasema ataondoa kinara chako, utaona hasara kwenye biashara yako, ataondoa ile nuru katika biashara yako kwasababu umejua umekosa na haujataka kurudi kwenye nafasi yako.
Mungu ndiye kinara chako, ulikua mtoaji, leo huendi kanisani unasema michango mingi, biblia inatuambia
(1Wakorintho 16:1) ” Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.”
Tumeambiwa kuhusu habari ya changizo tuchange ipasavyo,

Utukufu wa Mungu unaoneka hata sasa – Ujenzi wa Kanisa kubwa unaoendelea kanisa la Efatha Kigoma mjini.

Hakika MUNGU wa Efatha ni MZURI sana, VIDEO inaonesha ujenzi wa Hema ya BWANA Ethatha Ministry Kigoma mjini. Ni baadhi tu ya MAMBO MAKUU anayotenda MUNGU ndani ya Huduma ya Efatha.

Huduma ya Efatha Kigoma chini ya Mchungaji Kiongozi BENSON MPELLE anawakaribisha watu wote katika Ibada mbalimbali zinazoendelea hapa kanisani.

RATIBA ZA IBADA NI KAMA IFUATAVYO

IBADA YA JUMPILI INAANZA: SAA 2:00 Asubuhi – 6:30 Mchana.

MAOMBI YA UPONYAJI NA UKOMBOZI JUMAMOSI: SAA 3:00 Asubuhi – 5:00 Asubuhi.

MADARASA YA WOKOVU NI JUMATATU NA ALHAMISI: SAA 10:00 Jioni – 12:00 Jioni.

Kwa msaada zaidi au ushauri wasiliana na Mchungaji kwa simu No:  0767 555 292

*** TAZAMA VIDEO YA UJENZI UNAOENDELEA EFATHA MINISTRY KIGOMA

 

Pichani CHINI: Mchungaji Kiongozi wa Efatha Ministry mkoa wa Kigoma na mkewe katika moja ya Ibada kanisani hapo.

 

Pichani CHINI: Kiongozi na mwanzilishi wa Huduma ya Efatha Duniani Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira (Katikati) akiwa na Mch. Kiongozi wa Efatha Ministry Kigoma pamoja na mkewe.

 

Pichani CHINI: Waimbaji wa mass choir Kigoma katika utumishi.