Posts

SOMO:TAMBUA NAFASI ULIYOPEWA NA UJIFUNZE KUAMINI MANENO YA MUNGU NAKUFUATA UTARATIBU WA KRISTO.

SEMINA YA NENO LA MUNGU GAIRO

NA MCHUNGAJI GLADNESS TUPA

Unaweza ukawa umeokoka lakini hauna utakatifu na unasema mimi nimeokoka. Mungu hawezi kumtumia mtu mbaye akili yake haiko vizuri. Kuna baadhi ya watu ambao Mungu anawatafuta ili awatumie. Mungu anawatafuta wale ambao wanamwabudu katika roho na kweli. Tatizo wewe hautaki kumpenda na kuishughulisha akili yako ndiyo maana Mungu hataki kukutumia. Jitoe kwa Bwana kwa chote chote kile ukisimama katika imani ya Kristo Yesu hautaona ugumu wowote. Unahitaji neema ya Mungu ili uweze kujitambua wewe ni nani siku zote za maisha yako unapoenda mbele za Mungu jitahidi sana kujua unamwendea Mungu gani katika maisha haya ya wokovu tunayopitia, tunaandaliwa kuwa wasaidizi wake.

2 WAKORINTHO 10: 1 Basi, mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu.

Usipofuata utaratibu wa maisha yako, utajisababishia adui kujivunia wewe katika utakatifu, kubali kufuata utaratibu amabo Mungu ametuwekea kupitia watumishi wake, pia Mungu anakuinulia mtu wakuja kukubadilisha ili ubarikiwe.

UJUMBE: JITENGE NA UOVU/DHAMBI

Mtu yeyote anayekubali kuokoka ni lazima akubali kuishi Maisha matakatifu wakati wote. Akubali kuikimbia dhambi kila wakati ndipo utapata kibali mbele za Mungu na unapoamua kuokoka ni lazima yale mambo ya kale yote uyaache maana wokovu ni jambo jipya linalofanyika ndani ya mtu. Ukiokoka unaacha yote ya kale na anaanza maisha mapya.

Kinywa chako siku zote kinene maneno yenye uzima ili uwe na mwenendo wa utakatifu. Unapaswa kutembea katika utakatifu ndiyo maana sisi tuliookoka tunauusiwa kutembea katika utakatifu. Kila mmoja wetu aliyeko humu ndani atembee katika utakatifu kwa kuushinda mwili wako ili usinajisike achana na dhambi ya kumsema mwenzako, kumnenea mabaya na jitahidi kushinda mwenendo wako.

Enenda na mwenendo wa Kristo ili upate kuheshimika. Yamikini tabia na mwenendo wa mwili wako ndiyo unaosababisha hayo maumivu unayopitia leo, hivyo katika kizazi hiki cha leo ni lazima ushinde mwenendo wa mwili na Mtu aliyeshinda mwenendo wa mwili unaona mafanikio yake ,ukishinda mwenendo wa mwili matakatifu yatakuwa ya kwako.

Zaburi 4:4 Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya; Mtu mwovu hatakaa kwako;

Muwe na hofu wala msitende dhambi ukitenda dhambi unakuwa unapoteza utakatifu wako,hivyo wakati wote katika wokovu wako tafuta utakatifu na wala usimpe ibilisi nafasi katika maisha yako.
Nguvu ya Mungu haiwezi kukaa kwa mtu ambaye hatembei katika utakatifu.

MCHUNGAJI GLADNESS TUPA

UJUMBE: TAFUTA USHIRIKA NA YESU. – Efatha Morogoro

MCHUNGAJI GLADNESS TUPA.


1KOR 1:1 “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo”.

Mtu yeyote ambaye anapenda ushirika mzuri na YESU lazima anakuwa karibu na YESU. Mtu yeyote anayekuwa na utakatifu ndani yake anakuwa na ile nguvu ya kuifanya kazi ya MUNGU. Anakua na neema ya kujitoa kwa nguvu, mali, Roho, mwili, muda, na akili yake tena bila kunung’unika tena anakuwa tayari . Mtu wa namna hii siyo rahisi amtumikie shetani lazima atampinga kwa nguvu zake zote. Na yeyote anyefanya mambo hayo lazima anakuwa na matokeo mazuri na ni mtu ambaye yuko tayari kujitolea hata kisadaka. Na kwa kuwa ni mtakatifu hayoko tayari kumkosea mtakatifu wala kumkosea MUNGU.
Ukiwa na Roho ya kumkaribia BWANA kila wakati itakulinda. Roho ya ibada ni ya muhimu sana kwako wewe ambaye una safari ya kwenda mbinguni. Mtu yeyote anayepata mafundisho ya kitume akayazingatia na kutendea kazi ni rahisi sana kupata majibu kwa yale anayotaka kutoka kwa MUNGU wake na majibu yanatokana na ushirika wake na MUNGU.

Ushirika wa mtu aliyeokoka na MUNGU unaambatana na neno la uaminifu. Unaonaje ukawa mwaminifu kwa yale unayofundishwa na kuelekezwa. Chochote unachoelekweza, unachofundiswha na unachoonywa; unapokuwa mwaminifu ndipo unaruhusu ile neema ya ki-Mungu ikae ndani yako maana MUNGU anatafuta mtu mwenye akili nzuri aweze kumtumia. Ili aweke baraka zake kwako, ili aweke roho ya ibada kwake na mafanikio na akishamuweka inakua ni kwa faida ya wengine siyo kwa faida yake, ndiyo maana tunasema uwahurumie na wengine kwa kuwashuhudia. Hiki unachopewa ni kwa ajili ya ndugu zako, rafiki zako, jamaa yako na wafanya kazi wenzako. Yesu akasema enendeni duniani kote mkaihubiri injili kwa mataifa yote.