Posts

USHUHUDA: (Mungu amempatia watoto baada ya kuokoka hapa Efatha)

Efatha Ministry Mwenge DSM

Naitwa Rebeka Chaula, nilikuwa na shida ya kupata mtoto kwa muda mrefu nikaenda Hospitali Mwananyamala nikaambiwa nina uvimbe na nikaenda mara ya pili wakasema nina tatizo kubwa nikaambiwa niende Muhimbili. Na kabla ya kwenda huko nikamwambia mume wangu nataka nitafute Kanisa nitakaloenda kuombewa na kupona mume wangu hakuamini.

Nikakumbuka nilikuwa naangalia TRENET TV nikawa namuona Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiombea watu na nikasema hili Kanisa ndiko nitakapo kwenda kupona, Jumapili ilipofika niliamua kuja hapa Efatha na walipoita watu wanaotaka kuokoka nikatoka mbele kuokoka na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Mwingira akaniombea akasema tatizo langu limeisha akanikabidhi kwa askofu wakunilea. Baada ya hapo nikapata ujauzito na nikajifungua salama.

Mtoto wa pili nikaambiwa natakiwa kujifungua kwa upasuaji nikasema kwa Yesu wa Efatha hakuna upasuaji na baada ya muda kidogo nikajifungua kwa njia ya kawaida na leo nina watoto wawili. Namshukuru sana Mungu wa Efatha kwa matendo makuu aliyonitendea.

SHUHUDA (Uponyaji wa tatizo la tumbo lililomsumbua muda mrefu)

NAITWA VALENTINE MWINGIRA. – Kutoka Efatha Ministry Ruvuma

Napenda kumuaibisha shetani amenitesa sana, kila siku nilikua namlilia Mungu aniponye maana nilikua natapika damu kuanzia mwaka 2013, nimezunguka hospital nyingi sana mpaka muhimbili, nikaambiwa nina vidonda kifuani, ikanilazimu nifanyiwe upasuaji zaidi ya mara mbili lakini bado tatizo lilibaki vile vile ,niliendelea kutapika muda mwingine nilipoteza fahamu, vipimo vilionyesha nina apendex iliyooza, utumbo wote umejaa na usaha na unatoa harufu madaktari wakashangaa nawezaje kuishi wakati tumbo lote limeoza baadae wakaniuliza mtume na nabii JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA ni nani yako? nikawaambia ni kaka yangu wakasema ndio maana upo hai mpaka leo. Namshukuru Mungu amejibu maombi yangu, hakuniacha nife japo wengi walisema siwezi kuishi tena, sasa mimi ni mzima tatizo langu limeisha sitapiki tena damu namshukuru Mungu kwa kuniponya. Mungu wa Efatha anaweza jamani..

USHUHUDA Kutoka Efatha Ministry Kilimanjaro KDC

Naitwa Charles Mdage naishi mwanga ilikuwa siku ya jumapili nilikuwa nimetoka kazini nikapanda gari ya kurudi nyumbani baada ya kufuka njia panda gari likaanza kuyumba kuelekea darajani nilianza kuomba na kujifunika kwa damu ya Yesu lile gari likagongana na noah upande ambao nilikuwa nimekaa.

Watu wakaanza kupiga kelele na mistuko ya hapa na pale lakini ashukuriwe Mungu wa Efatha kwa sababu niitoka nikiwa mzima wa afya na mpaka sasa ninaendelea mbele nakusihii mwana wa Mungu chochote kile unachokifanya kazi au safari mwambie Mungu aende nawe, tuache mazoea wewe usiende mwenyewe kwa sababu ukienda mwenyewe hautafika SALAMA.