UJUMBE : AMUA, SEMA, TENDA KWA USAHIHI – KUSANYIKO KUU LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA

PASTOR GARY WINSTON-USA

Mungu haonyeshi mapenzi yake kwako bali wewe ndio unapaswa uonyeshe mapenzi yako kwake. Kama unataka kuyaona mapenzi ya Mungu katika maisha yako angalia maisha yako, unakula unatembea, unapumua maisha yako yote ni mapenzi ya Mungu, hivyo sasa unapaswa wewe kuonyesha mapenzi yako kwake.
Jitangazie “Mimi nitayaonyesha au nitayathibitisha mapenzi ya Mungu katika maisha yangu”

Usifike mahali ukasema Ibilisi ananifuatilia sema mimi ninayaangusha malango ya Ibilisi, yaani usiwe na hofu wala mashaka.
Unapokutana na hali yeyote ile ya kukuangusha au kukufanya uwe chini je unatakiwa kufanyaje? Unapaswa kusimama kwa ujasiri. Kuanzia leo hakuna jambo litakalo kuzuia kwa Jina la Yesu. Lakini ili hayo yaweze kutokea kwako unapaswa usimame kwa ujasiri na uchukue hatua, kwa kufanya hivyo kila kitu ambacho kilikuwa kinakusumbua kita inama mbele zako.

Comments

comments

Comments are closed.