UJUMBE: NEEMA YA MUNGU (MCH. BONIFACE EVARIST – EFATHA MINISTRY MBINGA)

NEEMA NI NINI?
Neema ni msukumo wa kiungu ndani ya moyo wa mtu na unaookana au kuoneshwa kwa nje. Kwa maneno mengine, naweza kusema neema ni kibali ambacho hukustahili. Neema inaleta uzuri “Mithali 4:9 Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji ya uzuri.”
Kuongezeka katika neema, yaani kukua kunatokana na pale tunapokuwa na kumjua sana Bwana wetu. Usiwe kinyume na neema inayoonekana ndani ya watu wengine; tambua neema yao, heshima na saidia kuikuza unapoona inaonekana ndani ya mtu aliye karibu nawe.
Efeso 2:8-9. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Yohana 15: 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

Isaya 41:13 Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.

Yohana 10: 28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. 29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

2 Peter 3:18” Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.

KAZI SABA (7) ZA NEEMA
Neema ya Mungu inaonekana katika kile inazalisha; inajidhihirisha yenyewe kwa nje ya mtu aliye nayo kwa namna mbalimbali:

1. KIBALI
Neema inaleta KIBALI. Mambo mema yanakuja kwa mtu mwenye neema na msamaha wa Mungu muda wote uko juu yake. Hata kama mtu anaonekana alifanya makosa makubwa, ile neema ya Mungu inanena kwa niaba yake. Kutembea katika neema maana yake ni kutembea ushawishi wa Kimungu. Inakufanya utembee na ufahamu huu “kwamba kama nataka kitu nitakipata”. Maana Mungu anataka kuonesha ulimwengu kwamba kila mtu ajue kuwa wewe unapendwa na Mungu. Hakuna tena kahangaika sana na mashaka yanasinyaa. Neema ipo kwa ajili ya kukupa kibali wewe. Anachotaka Mungu ni ujitoe kwake.

2. KUKUBALIKA
Mtu mwenye neema daima anavutia watu kwake. Neema inakuweka mpendwa, na watu wanakuwa hawaelewe kwa nini wana vutiwa na wewe. Neema haiangalii cheo cha mtu, ujuzi au jinsia. Unaweza kuingia katika neema ya Mungu maishani mwako. Mungu anakuongezea neema pale anapoona ile neema uliyonayo sasa unaitumia. Neema husababisha Mazingira kuitikia au kukubaliana na wewe. Na kuna viwango vingi vya neema. Ninatamani uwe mmoja wa watu ambao watatembelea kiwango cha juu cha Neema.

3. FAIDA
Neema inakuletea na inakupa wewe faida. Wewe Mkristo unatakiwa DAIMA uwe na ufahamu wa neema ya Mungu juu ya maisha yako, ndipo itakapo fanya kazi kwako. Huhitaji kahangaika na chochote katika maisha yako kama utaifanya neema iwe kazini, itakuletea kile utakacho

4. FURAHA
Neema huleta furaha; furaha isiyoelezeka wala kupimika. Kwa yule anayetembea katika neema furaha inajaa maisha yake yote. Hii pia ni faida ya neema ambayo inakufanya usione kile wengine wanazungumza wakilalamikia Serikali, Mazingira na magonjwa pia. Pale wengine wanapokuletea huzuni na mambo ya kusikitisha, wanaanza kushangaa wewe unakuwa mgawaji wa furaha. Ukishakuwa na neema katika maisha yako hakuna magumu kwako hata kama upo katika matatizo makubwa. Pale changamoto zinapokuja kwako, angalia ndani yako ili upate suluhisho, kwa kuwa Unajua kwamba: TATIZO LIKIWA KUBWA, NDIVYO USHUHUDA UNAKUWA MKUBWA.

5. UKARIMU
Tambua kuwa mtu yeyote neema anakuwa mkarimu sana. Neema hufungua njia mbili yaani njia ya kutoa na njia ya kufungua. Tambua kuwa kutoa ni neema. Neema ikishafungua mlango wa kutoa; pia inafungua UWEZO wako wa kupokea.

6. PENDEZA
Neema inaleta kumpendeza. Neema ndiyo inayokupa kumpendeza katika yale yote ambayo Mungu ameumba. Maisha yako yote yapo kwa ajili Mungu; ukitambua hili tu unaanza kushangaa maisha yako ni ya kumpendeza sana na bado yanampendeza Mungu.

7. KARAMA
Ni neema inayokuletea KARAMA maishani mwako. Neema inaleta uwezo wa kufanya kile ambacho wengine hawawezi kufanya. Hii itatokea tu pale unapoanza kutambua ujuzi, ubora na ufahamu wa mambo fulani. Ni vema sana ukatambua kipawa cha Mungu ndani yako na ukaanza ukitumia. Inasababisha nguvu ya Mungu kuja juu ya kile kipawa.

HITIMISHO
WARUMI 6: 1 “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?”
Jibu lake: YOHANA 8:11 “Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.”
Zaidi sana, tuna kazi kubwa ya kufanya ili kwamba tutimize kusudi la kupewa Neema. Mungu anategemea sisi kuiongeza neema yake kwa kusoma kwa umakini na kutafakari Neno lake ambalo ni Neno la Neema.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *